Michakato ya kisemantiki katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili
Loading...
Date
2020
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es salaam
Abstract
Kisukuma ni miongoni mwa lugha za kibantu kama ilivyo Kiswahili, kimekopa maneno kutoka lugha mbalimbali za kibantu. Maneno hayo yanapokopwa hupitia michakato mbalimbali ili yafanane na mfumo wa lugha husika. Utafiti huu umechunguza michakato ya kisemantiki katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili. Ambayo wasukuma wanayatuimia kama sehemu ya msamiati wa lugha yao. Hali hiyo imesababisha baadhi ya maneno ya kisukuma yaliyokuwa yakitumika hapo mwanzo kuanza kupotea na nafasi za maneno hayo kukaliwa na manenoyenye asili ya Kiswahili. Tafiti nyingi zilizofanyika kuhusiana na michakato ya kisemantiki zina mwenga wa lugha za kigeni. Utafiti huu uliazimia kufanyika katika lugha zenye asili asili moja yani Kibantu pekee ili kubaini michakato inayojitokeza nan i mchakato upi unaongoza kuchakata data za lugha zenye asili moja ambazo ni Kiswahili na Kisukuma zote zikiwa ni lugha za kibantu. Utafiti huu ulilenga kubainisha michakato ya kisemantiki katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili na kulinganisha michakato ya kisemantiki iliyobainishwa katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili ili kubaini ni mchakato upi unaotawala zaidi . utafiti huu utatoa mwongozo kwa watafiti wanaotaka kuchunguza michakato ya kisemantiki katika lugha nyingine za kibantu. Nadharia ya maana kama matumizi ya Wittgenstein (1953) iliongoza utafiti huu. Msing mkuu wa nadharia hii ni kwamba, ni kosa kuyawekea maneno mipaka katika matumizi, kwani kufanya hivyo ni kuyawekea mipaka maumbo ya kiiisimu. Hivyo maana za maneno zitokane na mahitaji ya jamii husika inayotumia maneno hayo. Maneno yaliyokopwa yametumika sawa na mahitaji ya jamii za Wasukuma. Eneo la utafiti lilikuwa mkoa wa Simiyu katika wilaya ya Busega kata ya Nyaluhande. Vijiji viwili vya Bdugu na Ng’wagindi viliteuliwa kuhakiki na kupata data nyingine za uhakiki zilizohitajika. Sampuli ya utafiti ilitokana na kundi la vijana 20 na wazee 20 wenye uwezo wa kuzungumza Kiswahili na Kisukuma. Utafitio huu ulitumia mbinu tatu ambazo ni mbinu ya maktabani, dodoso na mahojiano, data zilizokusanywa maktabani katika kamusi ya KKS (2013) toleo la tatu, kamusi ya Kisukuma yenye orodha ya maneno ya Kisukuma na kitabu cha dini nyimbo za sifa za Kisukuma (Mimbo). Data zilizokusanywa zilipelekwa uwandani kwa watoa taarifa kuhakikiwa kwa kutumia mbinu ya dodoso na majadiliano. Watafitiwa walipewa uhuru wakuondoa maneno ambayo hayakuwa ya mkopo kwa kuongeza mengine ambayo mtafiti hakuwa nayo. Utafiti ulitumia mkabala wa kimaelezo, data zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa data kimada na uchambuzi linganishi ili kurahisisha uchambuzi wake. Michakato minne ilibainishwa kuchakata data za lugha zenye asili moja ambayo ni MPK, MKK, MGK, MFK. Mchakato uliotawala zaidi ulibainishwa kuwa ni MFK ambao umeonekana kuchakata maneno mengi zaidi. Aidha, utafiti huu unapendekeza kuwa, tafiti fuatishi ziangalie michakato ya kisemantiki katika lugha nyingine za kibantu ili kuona hali inakuwaje katika lugha hizo.
Description
Available in print form, East Africana Collection ,Dr.Wilbert Chagula Library,Class mark (THS EAF P325.5H57T34L335)
Keywords
Semantiki, Sukuma, swahili, Language and Languages, Tanzania
Citation
Ladislaus P.K (2020). Michakato ya kisemantiki katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili. Tasnifu ya Udhamili