Ulinganishi wa sababu za kuanguka kwa shujaa katika utendi wa kiswahili na tendi nyingine za Kiafrika
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha na kulinganisha sababu za kuanguka kwa shujaa katika utendi wa Kiswahili na tendi nyingine za Kiafrika. Katika utafiti huu tumetafiti utendi wa Fumo Liyongo kwa upande wa utendi wa Kiswahili na tendi za Rukiza na Nyakiiru Kibi kwa upande wa tendi nyingine za Kiafrika. Katika kukusanya na kuchambua data tumetumia tendi teule na marejeleo mbalimbali kutoka maktabani. Mbinu ya uchambuzi wa matini, mkabala linganishi, nadharia ya mwitiko wa msomaji na nadharia ya naratolojia zimetumika katika utafiti huu kumsaidia mtafiti kutimiza malengo ya utafiti. Katika utafiti huu tumebaini kwamba kuanguka kwa shujaa wa utendi hutokana na sababu mbalimbali. Sababu hizo zinatokana na shujaa mwenyewe, jamii inayomzunguka, mazingira ya kimaumbile, mizimu au miungu. Katika Utendi wa Fumo Liyongo, Nyakiiru Kibi na Utendi wa Rukiza mtafiti amebaini kwamba sababu za kuanguka kwa shujaa ni tamaa ya madaraka, ushawishi, usaliti, tamaa ya mali, kutenguliwa kwa nguvu za sihiri, uzembe na udhaifu wa shujaa katika kufikiri na fitina. Hivyo, utafiti huu unaonesha kwamba sababu za kuanguka kwa shujaa katika utendi wa Kiswahili na tendi nyingine za Kiafrika zinafanana. Matokeo haya ya utafiti yamejikita katika utendi wa Fumo Liyongo, Nyakiiru Kibi na Rukiza. Tafiti nyingine zifanywe katika tendi nyingine za Kiafrika na tendi za mataifa mengine ili kubaini kama sababu za kuanguka kwa shujaa zinafanana au hazifanani.