Usawiri wa wahusika wa kike katika hadithi fupi za watoto za kiswahili
dc.contributor.author | Mhawili, Angela Peter | |
dc.date.accessioned | 2020-04-01T08:00:50Z | |
dc.date.available | 2020-04-01T08:00:50Z | |
dc.date.issued | 2012 | |
dc.description | Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.A2M4752) | en_US |
dc.description.abstract | Utaflti huu unashughulikia usawiri wa uhusika wa wanawake katika hadithi fupi za watoto za Kiswahili. Tatizo lililotusukuma kuitafiti mada hiyo linatokana na ukweli kwamba usawiri wa wanawake katika hadithi fupi za watoto haujaguswa bado. Ingawa watoto ni sehemu muhimu ya jamii na ndio wanaohitajika katika kubadili na kuijenga upya jamii, bado suala la malezi yao halijatambulika na kufanyiwa uchunguzi wa kina. Ili kubaini na kuweka wazi suala la malezi ya watoto, tasnifu hii imejikita katika kutafiti juu ya usawiri wa wahusika wa kike katika hadithi fupi za watoto. Hadithi zilizotumika kuchambua tatizo la utaflti zinatoka katika Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania. Ili kuyatimiza malengo ya utaflti husika, marejeo mbalimbali yalitumika kutoka maktabani. Hivyo utaflti huu ulikuwa wa maktabani. Pia nyenzo za kama vile kompyuta, kalamu na kalatasi, zilitumika katika kukusanyia na kuchambulia data. Mbali na mbinu hizi, mtafiti aliongozwa na nadharia za Mtazamo-Kike kama ilivyorejelewa na Njogu na Chimerah (2008). Katika tasnifu hii imebainika kuwa suala la unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia kwa mtoto wa kike na mwanamke limejitokeza pia katika hadithi fupi za watoto. Tasnifu hii imependekeza kuwa, ili kuibadilisha jamii kutokana na mitazamo potofu dhidi ya jinsia ya kike, na kujenga jamii yenye kufuata misingi ya haki na usawa kwa jinsia zote, watunzi wa kazi za fasihi ya Kiswahili kwa watoto washiriki katika suala la malezi ya watoto kwa kuonyesha usawa wa jinsia kwa wahusika wote. | en_US |
dc.identifier.citation | Mhawili, A P (2012) Usawiri wa wahusika wa kike katika hadithi fupi za watoto za kiswahili, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam | en_US |
dc.identifier.uri | http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/8660 | |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | University of Dar es Salaam, | en_US |
dc.subject | Short Stories | en_US |
dc.subject | Swahili | en_US |
dc.subject | Swahili language | en_US |
dc.subject | Women | en_US |
dc.title | Usawiri wa wahusika wa kike katika hadithi fupi za watoto za kiswahili | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |