Mandhari na shujaa wa kiutendi katika tendi za kiswahili: uchunguzi wa utendi wa Fumo Liyongo 1999 na utendi wa Nyakiiru Kibi 1997
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umechunguza mandhari na shujaa wa kiutendi katika tendi za Kiswahili. Uchunguzi wa Utendi wa Fumo Liyongo na Utendi wa Nyakiiru Kibi. Vigezo an sifa za kumbaini shujaa wa kiutendi vimeelezwa kwa kupitia wataalamu mbalimbali wa fasihi ya Kiswahili. Aidha, miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na watalaamu wengi wa fasihi havielekei kuitambua mandhari kama mojawapo ya vigezo muhimu vya kumtambulisha shujaa wa kiutendi. Hali hii ndiyo iliyohusukuma kuchunguza namna mandhari inavyoweza kumwibua shujaa wa kiutendi katika tendi za Kiswahili. Utafiti umeongozwa na malengo mahususi matatu: kubainisha mandhali zinazojitokeza katika Utendi wa Fumo Liyongo na Utendi wa Nyakiiru Kibi, kuchunguza namna mandhari zinavofungamana na shujaa wa kiutendi katika Utendi wa Fumo Liyongo 1999 na Utendi wa Nyakiiru Kibi 1997, na kuchambua namna mandhari inavyompambanua shujaa wa kiutendi katika Utendi wa Fumo Liyongo na Utendi wa Fumo Liyongo Kibi. Utafiti huu ulingozwa na nadharia mbili yaani Nadharia ya Uhalisia iliyoasisiwa na Hegel na waitifaki ni Georg Lukacs (1972) na wengine. Nadharia nyingine ni ya Uhalisiamazingaombwe iliyoasisiwa na Franz Roh (1925). Sambamba na hiyo, mkabala wa kitaamuli ulitumila katika kuchambua na kuwasilisha data. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwapo kwa mandhari halisi na mandhari isiyohalisi katika tendi teule. Vilevile, utafiti umebainisha kwamba, shujaa wa kiutendi anafungamana na mandhari katika kifo chake, safari yake, kusalitiwa kwake, katika kuishi kwake, katika kukua kwake, katika mapambano yake. Mwisho, utafiti umebaini kwamba, mandhari imempambanua shujaa wa kiutendi kama mtu shupavu na jasiri; shujaa ni mtu ambaye kifo chake hutokana na visa na kusalitiwa, shujaa ni mtu asiyeweza kudhurika kirahisi, shujaa ni mtu asiyeweza kufa bila sihiri yake kuguswa. Kwa ujumla, matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba mandhari ni kigezo na sifa muhimu katika utendaji wa shujaa wa kiutendi. Inapendekezwa kwamba wanataaluma wamakinikie kipengele cha mandhari kwa kina zaidi katika uwanja wa tendi ili kuweza kupanua uga wa uelewa wa mandhari katika tendi za Kiswahili kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.