Matumizi ya neno “shikamoo” katika mtandao wa jamii forums: uchunguzi wa maana yake kimuktadha.

dc.contributor.authorWilliam, Daud
dc.date.accessioned2020-04-20T10:29:44Z
dc.date.available2020-04-20T10:29:44Z
dc.date.issued2018
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.T34W544)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu maana ya neno “Shikamoo” kulingana na muktadha wa matumizi yake katika mtandao wa JamiiForums. Jumla ya majukwaa 12 ya mtandao huo yamehusishwa katika utafiti huu. Eneo letu la kiutafiti ni mtandao wa JamiiForums. Data ya utafiti huu imekusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi matini. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Maana kama Matumizi ya Ludwig Wittgenstein (1953). Mkabala wa kimaelezo ndio uliotumika katika uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa kuna matumizi ya aina saba ya neno “Shikamoo” katika mtandao wa JamiiForums kutokana na jinsi lilivyotumiwa. Pia, imebainika kuwa neno “Shikamoo” limetumiwa katika miktadha nane ya kimatumizi. Kutokana na miktadha hiyo, neno “Shikamoo” limechanuza maana nane za kimuktadha. Kutokana na neno hilo kuchanuza maana nane tofautitofauti zinazotokana na muktadha wa kimatumizi, utafiti huu unapendekeza kuwa maana za neno hili pamoja na maneno mengine katika lugha, fasili zake katika kamusi zitolewe kwa kuzingatia miktadha ya kimatumizi. Kufanya hivyo, kutawasaidia wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili kung’amua maana na kutumia maneno kama hayo katika muktadha husika. Aidha, tafiti nyingine zinaweza kuchunguza miktadha ya matumizi ya maneno mengine kwa kuwa miktadha ni mingi na huendelea kuzaliwa kila siku kutokana na maendeleo ya jamii.en_US
dc.identifier.citationWilliam, D. (2018). Matumizi ya neno “shikamoo” katika mtandao wa jamii forums: uchunguzi wa maana yake kimuktadha. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9615
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectDictionaryen_US
dc.subjectJamii Forumsen_US
dc.subjectShikamooen_US
dc.titleMatumizi ya neno “shikamoo” katika mtandao wa jamii forums: uchunguzi wa maana yake kimuktadha.en_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
William 2018.pdf
Size:
364.84 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: