Thari ya lugha katika kuibua dhamira: mifano kutoka nyimbo za kizazi kipya zihusuzo Ukimwi

Date

2011

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Kazi hii imelenga katika kuchunguza athari ya lugha ya kisanaa katika kuibua dhamira mifano ikitolewa kutoka nyimbo za Kizazi Kipya (Bongo Fleva) zinazohusu UKIMWI. Lugha ya Kisanaa ni ile ambayo mtunzi wa kazi ya fasihi huitumia katika kuijenga kazi yake na kuitofautisha na kazi nyingine ya maandishi. Ni lugha ya kiubunifu yenye wingi wa tamathali za semi, picha, taswira, methali na nahau. Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa ni, kubainisha na kufafanua namna lugha ya kisanaa kutoka nyimbo za Bongo Fleva inavyosaidia kuibua dhamira na kugusa mwitiko wa jamii kuhusu UKIMWI. Ili kufanikisha utafiti huu, Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji imetumika, lengo likiwa ni kubaini mwitiko wa wasomaji au wasikilizaji juu ya dhana mbalimbali ambazo zimetumika katika nyimbo za Bongo Fleva zilizohusu UKIMWI. Njia za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji data ni zile za maktaba na uwandani. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji data ni hojaji, maswali ya mwongozo na tepu rekoda. Kwa jumla matokeo ya uchanganuzi data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha kuwa vipengele vya lugha ya kisanaa vinasaidia kuibua dhamira mbalimbali na vinagusa hisia za wasikilizaji na hata kusababisha mwitiko wao kuhusiana na UKIMWI licha ya athari za kawaida za kuburudisha na kuelimisha. Matumizi haya ya lugha yanaweza kujenga mwitiko unaoweza hatimaye kutokeza mabadiliko ya kitabia na hivyo kuweza kuzuia kuenea kwa VVU.

Description

Available in print

Keywords

Swahili language, Bongo fleva

Citation

Low, N. R. (2011) Thari ya lugha katika kuibua dhamira: mifano kutoka nyimbo za kizazi kipya zihusuzo Ukimwi. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx