Mchango wa tendi katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu lilikua kuchunguza mchango wa tendi katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Katika kulikamilisha lengo hili mtafiti alishughulika malengo mahususi matatu ambayo yalikuwa ni kubainisha vipengele vya kifani na kimaudhui vya tendi. Pili kuonyesha jinsi vipengele hivyo vya kiutendi vinavyobainika katika riwaya teule za Kiswahili na lengo la mwisho lilikuwa ni kueleza mchango wa mwingiliano huo katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Ili kutimiza malengo hayo, utafiti huu umefanyika katika Maktaba Maktaba Kuu ya chuo kikuu cha Dar es salaam na makavazi ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI).Mbinu za utafiti zilizotumika ni ukusanyaji matini na udurusu matini katika kukusanya data za msingi pamoja na data za upili. Katika uchambuzi wa data mtafiti alitumia mkabala wa kimaelezo usiokuwa wa kiidadi na nadharia iliyotumika ni nadharia ya mwingiliano matini. Matokeo ya utafiti huu yametimiza malengo yaliyokusudiwa. Mtafiti ameweza kubainisha vipengele vya utendi vya kifani na kimaudhui na kuonyesha jinsi vipengele hivyo vya tendi vinavyoingiliana na riwaya teule za Kiswahili. Mwisho mtafiti ameweza kuonyesha mchango wa mwingiliano huo katika riwaya ya Kiswahili. Mtafiti amedhihirisha kuwa waandishi wa riwaya ya Kiswahili wamekuwa wakitumia wakitumia vipengele vya kifani na kimaudhui vya utendi kwa kujua au bila kujua. Vilevile kuna maeneo ambayo yamependekezwa na utafiti huu kwa ajili ya tafiti zijazo. Maeneo hayo ni utafiti kuhusu mchango wa tendi katika aina nyingine ya riwaya ya Kiswahili kwa sababu utafiti huu ulijikita katika riwaya nne tu pili, utafiti kuhusu tanzu nyingine za fasihi andishi zinavyoingiliana na tendi. Hivyo, mwingiliano huo umetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili.