Matumizi ya mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi kwa lugha ya Kiswahili katika redio mifano kutoka vipindi vya burudani

Date

2013

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Ili kutekeleza wajibu wao wanahabari hutumia mitindo mbalimbali ya lugha katika vipindi vyao vya redio. Hata hivyo ni wataalamu wachache sana waliotafiti ni kwa namna gani mitindo ya lugha hutumiwa katika redio. Ili kujaribu kuziba pengo hilo, utafiti huu umeshughulikia namna mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi kwa lugha ya Kiswahili unavyotumika katika vipindi vya redio vya burudani nchini Tanzania. Utafiti ulilenga; mosi, kubainisha nafasi ya mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi katika vipindi vya redio vya burudani. Pili, kuainisha na kufafanua sifa za kiisimu za mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi kwa lugha ya Kiswahili katika vipindi vya redio vya burudani. Tatu, kueleza sababu zinazosababisha matumizi ya mtindo huo wa lugha katika vipindi vya redio vya burudani. Utafiti uliongozwa na nadharia ya mtazamo wa wasikilizaji iliyoasisiwa na Allan Bell mwaka 1984. Mbinu za mahojiano, hojaji na mbinu ya kusikiliza zilitumiwa na mtafiti kupata data zilizohitajika. Aidha, Mikabala ya kimaelezo na kiidadi imetumika katika uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo. Matokeo hayo pamoja na mambo mengine, yamedhihirisha kuwepo kwa sifa za kiisimu zinazo upambanua mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi kama unavyotumika katika vipindi vya redio vya burudani. Sifa hizo ni pamoja na matumizi makubwa ya msamiati unaotokana na misimu. Aidha, imedhihirika kuwa zipo sababu zinazofanya mtindo huo wa lugha utumike katika vipindi vya redio vya burudani. Moja ya sababu hizo ni haja ya kuwaridhisha wasikilizaji walengwa wa vipindi hivyo. Inapendekezwa mtindo huo wa lugha uendelee kutumiwa katika vipindi vya redio vya burudani.

Description

Keywords

Style, Swahili language

Citation

Kihombo, M (2013) Matumizi ya mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi kwa lugha ya Kiswahili katika redio mifano kutoka vipindi vya burudani, Tasinifu ya M.A. (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)