Utohozi wa istilahu za kiingereza katika Kiswahili: uchunguzi kifani wa taaluma za tiba na compyuta

dc.contributor.authorAdolph, Editha
dc.date.accessioned2021-10-11T12:28:20Z
dc.date.available2021-10-11T12:28:20Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionAvailable in print form,East Africana Collection ,Dr.Wilbert Chagula Library,Class mark ( THS EAF PL8703.A364)en_US
dc.description.abstractKila lugha huwa na utaratibu wake wa ukuzaji na uendelezaji wa msamiati. Katika mchakato wa kupata msamiati wa lugha husika, mbinu mbalimbali hutumika. Utohozi ni mbinu moja wapo ambayo lugha hutumia katika kujitajirisha kimsamiati. Ili msamiati uweze kukubalika katika mbinu hii, kuna michakato mbalimbali inayopitiwa. Michakato hiyo huweza kusababisha athari katika lugha pokezi. Utafiti huu umechunguza utohozi wa istilahi za fani ya tiba na kompyuta za kiingereza katika lugha ya Kiswahili kwa kuangazia michakato na athari zake. Utafiti umefanyika katika jiji la Dar es Salaam hususan katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kilichoko Wilaya ya Ubungo pamoja na baraza la Kiswahili la taifa lililopo wilaya ya Kinondoni. Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni nadharia ya Fonolojia Zalishi (NFZ) iliyoasisiwa na Naomi Chomsky na Moris Halle (1968) pamoja na andharia ya mofolojia Leksika (NML). Ambayo mwasisi wake ni Kiparsky (1982). Aidha, data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji na uchambuzi wa matini. Data iliyokusanywa ilichambuliwa kwa kutumia mkataba wa maelezo na wa kitakwimu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa lugha ya Kiswahili imetoa istilahi za fani ya tiba na kompyuta kutoka katika kiingereza. Pia, utafiti umebaini kuwa wakati wa utohozi wa istilahi katika Kiswahili, michakato mbalimbali ya kifonolojia, kimofolojia na kisintaksia hufanyika. Michakato hufanyika kadiri kanuni na taratibu za lugha ya Kiswahili ili istilahi ziweze kukubalika. Michakato ya kifonolojia iliyobainishwa katika utafiti huu ni pamoja na mchakato wa udondoshaji, uchopekaji, usahilishaji wa irabu uangalifu kuwa irabu sahili na mchakato wa ufupishaji wa irabu ndefu. Michakato ya kimofolojia iliyoonekana kutokana na uchambuzi wa data ni pamoja na uambishaji ambao unafungamana na upangaji wa istilah za Kiingereza katika ngeli za Kiswahili uchakataji wa istilahi zenye muundo wa maneno ambatani Kisintaksia, imabainika kuwa istilahi hutoholewa kwa kuhusisha mchakato wa kuchopeka vihusishi kati ya istilahi za Kiingereza. Halikadhalika, utafiti huu umebaini kuwa utohozi wa istilahi za fani ya tiba na kompyuta za kiingereza za kiingereza katika Kiswahili una athari chanya na hasi katika lugha ya Kiswahili. Athari chanya zilizobainika ni pamoja na zile za kifonolojia, kisemantiki na kileksia. Athari za kifonolojia zilizoonekana katika utafiti huu ni pamoja na muundo mpya wa silabi katika Kiswahili na athari za kimatamshi zinazoambatana na ufifishaji wa sauti. Athari za kisemantiki zilizobainika ni pamoja na upatikanaji wa dhana za kisayansi pamoja na visawe vinavyotokana na utohozi. Kwa upande wa athari za kileksika, imedhihirika kuwa baadhi ya istilahi za fani za tiba ya compyuta zimeonekana kuongezeka katika Kiswahili. Athari hasi zilizobainika ni pamoja na pamoja na zile za kimofolojia, kisemantiki na kileksika. Kimofolojia imeonekana kuwa utohozi umesababisha muundo wa istilahi ndefu na zenye kutatanisha katika matamshi. Halikadhalika, Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kisemantiki kumezuka mfumuko wa visawe katika Kiswahili. Kileksika imebainika kuwa zipo istilahi za tiba na kompyuta zinazotumika mara chache. Utafiti huu umependekeza kwamba utohozi wa istilah za lugha mbalimbali ufuate kanuni na taratibu zinazowekwa katika Kiswahili. Aidha kuna haja ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kutumia istilahi za Kiswahili hata kama kuna istilahi zinazotoholewa. Hivyo mtafiti anapendekeza kuwa pawepo na uhamasishaji wa matumizi ya istilah za Kiswahili zilizopo ili kuepuka mfumko wa istilahi nyingi zinazorejelea dhana moja. Mtafiti kuwa kuna haja ya kufanya uchunguzi zaidi kuhusu utohozi wa istilahi za kiingereza katika Kiswahili kwa miaka ijayo kwa kuwa ni bayana kuwa mchakato wa utohozi ni endelevu.en_US
dc.identifier.citationAdolph, E (2019) Utohozi wa istilahu za kiingereza katika Kiswahili: uchunguzi kifani wa taaluma za tiba na compyuta. Tasnifu ya Udhamili (Kiswahili). University of Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15983
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectMedicineen_US
dc.subjectEnglish languageen_US
dc.subjectKompyuta languageen_US
dc.titleUtohozi wa istilahu za kiingereza katika Kiswahili: uchunguzi kifani wa taaluma za tiba na compyutaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
EDITHA ADOLPH.pdf
Size:
7.81 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: