“Ulinganishi wa Kimakunduchi, Kimtende, Kibwejuu na Kikizimkazi”

Date

2011

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unajaribu kulinganisha Kimakunduchi, Kimtende, Kibwejuu na Kikizimkazi. Vipengele vilivyoshughulikiwa ni historia ya wenyeji wa vijiji vya Makunduchi, Mtende, Bwejuu na Kizimkazi. Aidha utafiti huu umetuonesha uhusiano wa historia na msamiati unaotumika na wenyeji wa Makunduchi, Mtende, Bwejuu na Kizimkazi. Tasnifu hii imegawika katika sura tano. Sura ya kwanza inatoa utangulizi wa jumla kwa kuelezea; usuli wa tatizo, tatizo, malengo, maswali, umuhimu, eneo na mawanda ya utafiti. Aidha, mapitio ya maandiko, kiunzi cha Nadharia, mbinu za utafiti na mpango wa uchambuzi wa data pia vimejadiliwa katika sura hii. Sura ya pili inajaribu kueleza historia ya watu wa Makunduchi, Mtende, Bwejuu na Kizimkazi. Vipengele vinavyoshughulikiwa ni historia ya Waswahili kwa ufupi, eneo linalohusika, historia ya Watu wa Makunduchi, historia ya Watu wa Mtende, historia ya Watu wa Bwejuu na historia ya Watu wa Kizimkazi. Uhusiano wa historia ya Makunduchi, Mtende, Bwejuu na Kizimkazi pia unajadiliwa humo. Sura ya tatu inalinganisha msamiati wa Kimakunduchi, Kimtende, Kibwejuu na Kikizimkazi. Aidha msamiati wa msingi na utamaduni umelinganishwa na kuoneshwa tofauti zake. Isitoshe katika sura hii mifano kadhaa ya usemaji wa Kimakunduchi, Kimtende, Kibwejuu na Kikizimkazi imetolewa. Sura ya nne inaonesha ulinganishi wa sauti za msamiati wa Kimakunduchi, Kimtende, Kibwejuu na Kikizimkazi. Sauti zilizodondoshwa na zilizobadilishana nafasi katika msamiati zimejadiliwa. Sura ya tano, inatoa muhutasari wa matokeo ya utafiti, mapendekezo ya utafiti na hitimisho.

Description

Available in print

Keywords

kae language, makunduchi language, Unguja, Zanzibar

Citation

Juma, M. A (2011) “Ulinganishi wa Kimakunduchi, Kimtende, Kibwejuu na Kikizimkazi”. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx