Matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam, nchini Tanzania: Uchunguzi kifani wa majina ya watu

dc.contributor.authorMadila, Zacharia
dc.date.accessioned2021-10-18T09:20:26Z
dc.date.available2021-10-18T09:20:26Z
dc.date.issued2020
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr.WilbertChagula Library, (THS EAF P323.T34M345)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam, nchini Tanzania. Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha kiwango cha matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam. Aidha, utafiti huu ulilenga kutathimini mitazamo ya wanajamii kuhusu matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam. Kadhalika, data ya utafiti huu ilikusanywa kwa njia ya usaili. Vilevile, utafiti huu umeshughulikiwa kiisimujamii kwa kuongozwa na Toleo la Wastani la Nadharia tete ya Uumbaji ya Sapir na Whorf ya mwaka 1958. Aidha data ya utafiti huu imechanganuliwakwa kutumia mkabala wa kitakwimu na kitaamuli. Hivyo kiwango cha matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam ni asilimia ishirini na sita nukta mbili tano (26.25%) ya majina yote yaliyokusanywa katika utafiti huu . Aidha, kiwango cha matumizi ya majina kutoka lugha zingine ni asilimia sabini na tatu nukta saba tano (73.75%) ya majina yote yaliyokusanywa katika utafiti huu. Kadhalika, asilimia hamsini na moja nukta nane saba tano (51.875%) ya watoataarifa wameona kuwa majian ya Kiswahili yatumike katika uteuzi wa majina ya watu jijini Dar es salaam ilihali asilimia kumi na sita nukta mbili tano (16.25%) ya watoataarifa wameona kuwa majina ya Kiswahili yatumike lakini majina teule yanapaswa kuwa na maana nzuri. Pia asilimia nne nukta tatu saba tano (4.375%) ya watoataarifa wameona kuwa lugha yoyote inaweza kutumika katika uteuzi wa majina. Kwea upande mwingine, asilimia ishirini na tatu nukta moja mbili tano (23.125%) ya watoataarifa wameona kuwa majina ya Kiswahili yasitumike. Hivyo, ingawa matumiza ya Kiswahili katika shughuli za kila siku jijini Dar es salaam yamewashawishi watoatarifa wengi waone kuwa kuna haja ya kutumia majina ya Kiswahili lakini kuna vipengele vya kiisimujamii kama maana mbaya za majina, kasumba ya kupenda majina kutoka lugha za kigeni na athari za dini ambavyo vimeukilia kiwango kidogo cha matumizi ya majina hayo. Aidha ,utafiti huu unatoa wito wa tafiti zijazo kufanyika kuhusu matumizi ya majina ya Kiswahili katika maeneo mengine nchini Tanzania. Pia, utafiti ufanyike kuhusu sababu na athari za ubadilishaji wa majina katika jamii. Kadhalika, utafiti mwingine ufanyike kuhusu nafasi ya Kiswahili katika uteuzi wa majina ya utani katika jamii.en_US
dc.identifier.citationMadila, Z (2020) Matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam, nchini Tanzania: Uchunguzi kifani wa majina ya watu, tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/16147
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectLanguagesen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectNamesen_US
dc.subjectDar es Salaamen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleMatumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam, nchini Tanzania: Uchunguzi kifani wa majina ya watuen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Zacharia Madila.pdf
Size:
6.34 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: