Muundo na dhima za vibainishi vioneshi katika kiswahili sanifu.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es salaam
Abstract
Utafitti huu ulinuia kuchunguza vibainishi vioneshi katika lugha ya Kiswahili ili kubaini muundo na dhima za vibainishi hivyo. Lengo hasa ilikuwa ni kujaribu kuondoa ukinzani wa hoja uliopo katika kuchanganua muundo na kudhukuru dhima za vibainishi vioneshi vioneshi ambapo mara nyingi wataalam huelezea dhima moja ya vibainishi ambayo nikuonesha msaafa ya ukaribu au umbali. Data za utafiti huu zilikusanywa maktabani kutoka katika matini za vitabu vya kichwamaji (kezilabai, 1974) na kivuli kinaishi (Mohamed,1990) Mbinu iliyotumika ni usomaji wa maandiko na kunukuu madondoo yanayohusiana na muundo na dhima za vibainishi vioneshi. Data hizo zilichambuliwa kwa mbinu ya maelezo. Nadharia ya mofolojia leksika iliyoasisiwa na Kiparsky (1982 ) ilitumika. kwa muhtasari, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba kuna miundo mitatu ya vibainishi vioneshi. Kwanza, kuna vibainishi vioneshi vya karibu na mzungumzaji vinavyoundwa na mzizi (h-) unaofuatiliwa na irabu iliyonakiliwa kutoka katika kiambishi ngeli cha kibainishi kinachohusika. Pili, kuna vibainishi viambishi vioneshi vya mbali na mzungumzaji ambavyo hutawaliwa na mzizi (h-) unaofuatiliwa na irabu ya kiambishi ngeli na kiambishi rejeshi (-0) mwishoni mwa vibainishi hivyo. Tatu, kuna vibainishi vioneshi vya mbali na mzungumzaji na msikilizaji, ambavyo huundwa na mzizi (-le) unaojitokeza mwishoni mwa kibainishi kinachohusika, ukitanguliwa na viambishi ngeli. Ama kuhusu dhima zilizobainishwa, ipo dhima ya kuonesha mahali ,dhima ya uhimizaji, msisitizo, kuuganisha, kuonesha umbali au ukaribu wa kitu na kuonesha mahali. Utafiti huu unapendekeza kwamba, utafiti mwingine kama huu unaweza kufanyika katika aina nyingine za vibainishi ili kupata maarifa majumui kuhusu muundo na dhima za vibainishi hivyo katika lugha ya Kiswahili, pia utafiti unaweza kufanywa kuchunguza muundo na dhima za vibainishi katika lugha mbalimbali za Kibantu ili kuona namna miundo na dhima zinavyoweza kutofautiana na/au kufanana na lugha ya Kiswahili.
Description
Available in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF P158.3.T34C425)
Keywords
Phrase structere grammar, Grammar, Language and languages, Linguistics, Swahili languages, Tanzania
Citation
Champunga, S. I. (2019) Muundo na dhima za vibainishi vioneshi katika kiswahili sanifu.tasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.