Utendeshi katika vitenzi vya lugha ya Kigweno

dc.contributor.authorMmary, Rizati Hassani
dc.date.accessioned2019-11-27T07:15:42Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:49Z
dc.date.available2019-11-27T07:15:42Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:49Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL 8228.24.M52)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu Utendeshi katika vitenzi vya lugha ya Kigweno uliofanyika katika mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania katika vijiji vya Vuchama, Mangio na Mwaniko. Tulitumia Nadharia ya Mazingira ya Utokeaji wa Alomofu ya Bobaljik (2000) katika kuchunguza mazingira yanayoukilia utokeaji wa maumbo yanayowakilisha mofimu ya utendeshi katika vitenzi vya lugha ya Kigweno. Nadharia nyingine ni ya Uhusiano wa Sauti- Maana- Kazi, ya Guthrie (1962) katika kushughulikia namna unyambulishaji wa utendeshi unavyokiathiri kitenzi kisintaksia. Pia tulitumia Nadharia ya Sarufi ya Utambuzi ya Langacker (1987) na Taylor (2003) katika kuchunguza maana zinazoukiliwa na uongezaji wa maumbo ya utendeshi katika vitenzi vya lugha ya Kigweno Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa maumbo yanayowakilisha alomofu za mofimu ya utendeshi katika lugha ya Kigweno ni: {-ith-}, {-eth-}, {-th-}, {-ish-}, {-esh-}, {-sh-}, {-t-} na {-r-}. Aidha, tumebaini kuwa unyambulishaji wa utendeshi unakiathiri kitenzi kisintaksia kwa kuongeza yambwa. Kwa upande wa maana tumebaini kuwa uongezaji wa maumbo ya utendeshi katika vitenzi vya lugha ya Kigweno kwa ujumla unaleta maana ya kusababisha au kumfanya mtu kufanya kitu. Kwa ujumla tumeainisha maana tabirifu na zisizo tabirifu. Tunapendekeza kuwa watafiti wengine wanaweza kuchunguza vitenzi nyambulishi vingine kama utendea, utendana, utendwa na utendeka.en_US
dc.identifier.citationMmary, R. H (2014) Utendeshi katika vitenzi vya lugha ya Kigweno, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3531
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectGweno languageen_US
dc.titleUtendeshi katika vitenzi vya lugha ya Kigwenoen_US
dc.typeThesisen_US

Files