Muundo na dhima ya vielezi katika Kiswahili
Loading...
Date
2016
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Abstract
Tasinifu hii I matokeo ya utafiti ulioshughulikia Muundo na Dhima ya vielezi katika Kiswahili, na imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia Tatizo la Utafiti na Kiunzi cha Nadharia kilichotumika katika uchambuzi wa mada. Sura ya pili imefenya mapitio ya maandiko mbalimbali yaliyoibua utafiti huu. Sura ya tatu imefafanua mbinu anuwai zilizotumika kuendesha utafiti huu. Sura ya nne imejihusisha na uchanganuzi wa data ulioibua mchango mpya wa utafiti huu, ambapo sura ya mwisho imefunga mjadakla kwa kutoa muhtasari wa tasinifu ya nzima na ushauri kwa utafiti mwingine unaoendana na utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu unaonesha kuwa, kimofolojia, vielezi vya Kiswahili vinaweza kuundwa kwa kuongeza {ki-}mwanzoni mwa baadhi ya nomino au vivumishi; kuongeza {ku-} mwanzoni mwa baadhi ya vimilikishi;kuongeza {vi-} mwanzoni mwa baadhi ya vivumishi; kuongeza kiunganishi {ni}mwishoni mwa baadhi ya nomino. Pia,vielezihuundwa na baadhi ya maneno ya uradidi, tanakali sauti, nomino za wakati, nomino za muekezo na baadhi ya maneno yasiyo na kategoria yoyote (vielezi asilia/ ushahidi). Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, kisintaksia,baadhi ya mafungu ya maneno hufanya kazi za uelezi, kama vile kirai elezi ambacho kinaweza kuundwa na kielezi peke yake; kielezi zaidi ya kimoja; mfano E + E, (anakula vizuri sana), E + E + E, (anampiga paka sokoni asubuhi mapema ); kielezi pamoja na kihusishi E + H, (anachuma maua juu ya mti ); E + E + H, (anafundisha somo vizuri sana mbele ya darasa); kirai husishi elezi (anacheza mpira kwa madaha). Pia kishazi elezi ambacho huundwa kwa kuanza na maneno ya viunganishi vinavyounganisha zaidi ya moja ndani ya sentesi moja, ambavyo vinachanuza utegemezi (kishazi tegemezi), kama vile japokuwa, ingawa, kwa sababu, kama, na mengine mengi: Mfano (Juma anakula chakula, ingawa anaumwa tumbo). Si hivyo tu, bali kisintaksia, utafiti umeonesha namna ya utokeaji wa vielezi katika tungo za Kiswahili kwa vielezi kuhamahama kwa kuwa mwanzo, kati au mwisho: (N + T + N + E), (N + T + E + N,) (E + N + T + N). kuhamahama huku kunategemea zaidi kama vielezi vinaelezea neno tu au sentensi nzima au mada, imegundulika kuwa mwenendo wa asili wa utokeaji vielezi ni kukaa baada ya mbwa lakini hutokea kukaa karibu na kijalizo chake (antecedent) na wakati mwingine hukubali kukaa mwanzoni mwa tungo. Matokeo ya utafiti huu yameonesha pia. Kisemantiki, vielezi vina dhina mbalimbali katika tungo za Kiswahili. Dhima kuu ya vielezi ni kueleza zaidi kuhusu kitenzi, vivumishi,kielezi na sentensi nzima kwa kukumisha umahali, uwakati, uidadi na unamna. Pia, utafiti umeeleza maana mahususi zinazojitokeza wakati vielezi vinapohamahama kwa kuwa mwanzo, kati au mwisho. Kwa ujumla, vielezi katika lugha ya Kiswahili vina miundo yake maalumu na dhima zinazojipambanua katika ligha ya Kiswahili tu.
Description
Available in print form,East Africana Collection ,Dr.Wilbert Chagula Library,Class mark ( THS EAF PL8702.A52)
Keywords
Swahili language, Grammar
Citation
Amanzi M.O (2016) Muundo na dhima ya vielezi katika Kiswahili,Tasnifu ya uzamiri,Chuo Kikuu cha Dar es salaam