Matumizi ya Kiswahili vijijini na athari zake katika lugha ya Kinyambo
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu unahusu matumizi ya Kiswahili na athari zake katika lugha ya Kinyambo. Utafiti uliongozwa na malengo matatu ambayo ni kubainisha nani anatumia Kinyambo na nani anatumia Kiswahili katika maeneo yaliyoteuliwa kwa kuzingatia umri na jinsi, kubainisha maeneo yanayotumia Kiswahili zaidi na maeneo yanayotumia Kinyambo na kujadili athari mbalimbali za matumizi ya Kiswahili katika Kinyambo. Aidha, Nadharia ya Uchanganuzi wa Kimaeneo ya Fishman (1972) imetumia kutoa mwongozo katika utafiti huu ambao umefanyika katika vijiji vya kakiro, Ruhanya na Chanika katika wilaya ya Karagwe, mkoa wa Kagera. Watoa taarifa 72 walihusika katika utafiti huu ambapo usampulishaji tabakisha ulitumika kwa kuzingatia umri na jinsi. Mbinu za hojaji, mahojiano na ushuhudiaji zilitumika katika ukusanyaji data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili inatumiwa na wazungumzaji wengi vijana na watu wa umri wa kati katika maeneo ambayo hapo awali yalitawaliwa na Kinyambo. Matumizi ya Kiswahili yamesababisha athari za kifonolojia, kimofolojia na kimsamiati katika lugha ya Kinyambo, jambo linaloashiria kupungua kwa matumizi ya Kinyambo kwa vizazi vijavyo. Utafiti huu unapendekeza kwamba asasi mbalimbali za serikali na binafsi zisisitize matumizi ya lugha ya Kinyambo katika mikutano ya hadhara, ibada na kwenye sherehe mbalimbali za kimila. Aidha, utafiti mwingine unaweza kuchunguza matumizi ya Kiswahili vijijini katika maeneo ambayo hayajafanyiwa utafiti kama vile michezo na burudani, matambiko, utawala na siasa ili kubaini kama yana athari zozote katika lugha za jamii.