Usawiri Wa Wahusika Vijalunga Katika Riwaya Ya Kiswahili:Mifano Kutoka Rosa Mistika Na Watoto Wa Mama N’tilie.

Date

2018

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo Kikuu cha Dar es salaam

Abstract

Utafiti ulichunguza uwasiri wa wahusika vijalunga katika riwaya ya Rosa Mistika iliyoandikwa kwa E. Kezilahabi (2000) na riwaya ya watoto wa mama n’tilie iliyoandikwa E.Mbogo (2008) na kuona jinsi wanavyokumbana na changamotokatika fasihi ya kiswhili na jamii kwa jumla. Utafiti ulilenga kubainisha matendo ya wahusika vijalunga katika riwaya teule, kubainisha kauli walizochorwa nazo wahusika vijalunga katika riwaya teule, kubainisha changamoto zinazo wakabili vijalunga ndicho kilichoshughulikiwa na kazi hii. Wahusika vijalunga ni aina ya wahusika walioko kati ya umri wa miaka hadi 9 hadi 19 wahusika hawa hutumika katika fasihi ili kuonesha mwenendo wa kundi - rika hili katika jamii husika. Utafiti Ulitumia Nadharia ya Uhalisia, inayoieleza fasihi kama Sanaainayoakisi uhalisia uliopo nje ya Sanaa. Nadharia hii ilimsaidia mtafiti katika uchambuzi wa data kupitia riwaya teule. Utafiti ulisanifiwa katika kwa kujiegemeza katika mkabala wa kitaamuli. Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Hivyo, mbinu ya udurusu wa maandiko ndivyo ilivyotumika zaidi katika kukusanya data za utafiti. Pia, mtafiti alitumia mbinu ya usaili kwa baadhi ya wazazi na waandishi ilikupata tajiriba zaidi kuhusu vijarunga na riwaya husika jinsi waandishi waliyo wachora wahusika hao. Data zilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa misingi ya kitaamuli. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, wahusika vijalunga wanamatendo ya kipekee na kauli za kipekee kama vile: mihemko ya kingono, kujihusisha na mapenzi, wasichana kugombania wavulana, kutoa mimba, maamuzi ya haraka, utii wa woga, kushawishiana, wizi,kujihusisha na dawa za kulevya, kukatisha tamaa,kauli za mkato,mafumbo, kejeli na majigambo, pia, waandishi wamewasiri wahusika vijalunga wakikubana na changamoto kadhaa kama vile: kukosa malezi bora, kutoyafahamu mazingira yao yaliyo wazunguka, kupata mimba shuleni, kuambukizwa magonjwa, kutengwa na jamii, kukosa elimu, kuwa na halingumu ya kimaisha na kupoteza maisha. Asilimia kubwa ya changamoto zinazo wakumba vijalungazinatokana na ukosefu wa malezi bora kutoka kwa wazazi wao. Malezi yao huachiwa mama pekee bila ya msaada stahiki kutoka kwa baba. Matokeo hayo yatawanufaisha watafiti,walimu wa fasihi, wanafunzi na wadau wa fasihi ya Kiswahili kwa ujumla, Mwisho yametolewa mapendekezo yatakayoweza kusaidia kutatua changamoto zinazowakumba vijalunga kama vile kuwanao karibuna kuwashauri, kufuatilia nyendo zao, kuwapa elimu ya kijinsia, kuwapa elimuya stadi za maisha na kuweka kanuni katika malezi.

Description

Available in print form,East Africana Collection ,Dr.Wilbert Chagula Library,Class mark ( THS EAF PL 8702.M342)

Keywords

Swahili literature, Character and characteristics in literature, Fiction, Rosa mistica, Watoto wa maman`tilie, Tanzania

Citation

Makame M.I (2018) Usawiri Wa Wahusika Vijalunga Katika Riwaya Ya Kiswahili:Mifano Kutoka Rosa Mistika Na Watoto Wa Mama N’tilie,Tasnifu ya uzamivu,Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Dar es salaam