Usawiri wa falsafa ya kiafrika katika unyago wa jamii ya wamakonde: uchunguzi wa nyimbo za unyago wa Chiputu.

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu Usawiri wa Falsafa ya Kiafrika katika Unyago wa Jamii ya Wamakonde: Uchunguzi wa Nyimbo za Unyago wa Chiputu. Tatizo la utafiti lilitokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia yalivyobadilisha jamiihadi utanzu huu ukaanza kuonekana kuwaumepitwa na wakati na hauna maana. Utafiti huu ulifanywa ili kuonyesha kuwa unyago bado una dhima. Tulikusudia kuchunguza dhima mojawapo ya unyago wa jamii ya Wamakonde, ya kusawiri falsafa ya Kiafrika. Kwa hiyo, utafiti huu ulikuwa na malengo yakufafanua utendaji wa nyimbo katika unyago wa Wamakonde, kubainisha falsafa ya Kiafrika inayosawiriwa na nyimbo za unyago wa Chiputu wa Wamakonde, na mwisho kueleza dhima ya usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika nyimbo za unyago wa Wamakonde.Ili kufanya hayo, utafiti huu ulihusisha data zilizokusanywa uwandani kwa njia mbalimbali zinazojumuisha uchambuzi matini, ushuhudiaji wa kushiriki namahojiano huru. Aidha, utafiti wa maktabani ulisaidia kukamilisha malengo ya utafiti huu ambapo nyaraka mbalimbali kama vitabu, majarida vilidurusiwa. Katika uchambuzi na ufasiri wa data, nadharia ya Kijamii (Sosholojia ya Fasihi) ilitusaidia kuchunguza uhusiano wa unyago na imani za jamii inayohusika. Pia, nadharia ya Ontolojia ya Kibantu ilitumikakubainisha jinsi masuala yanayosawiriwa katika nyimbo za unyago wa Wamakonde.Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kuwa, kuna aina tatu za nyimbo za unyago wa chiputu kwa Wamakonde na kila kipindi kina utendaji wake.Nyimbo ambazo huimbwa kwa madhumuni ya kufundishia wari mambo mbalimbali na ambazo hubeba falsafa ya Kiafrika.Miongoni mwa falsafa hizo ni falsafa kuwa kifo si mwisho wakuwapo;falsafa kuhusu mizimu na nguvuzao katikakuwasaidia wanadamu; falsafa kuhusu Mungu na uwezo wake, na; falsafa kuhusu nafasi ya mwanamke na mwanamume katika jamii. Falsafa nyingine nikuhusu uzazi na malezi; falsafa kuhusu imani za uchawi, uganga na sihiri; falsafa kuhusu utu;na falsafa kuhusu heshima kwa wakubwa. Pia, imebainika kuwa usawiri huu wa falsafa ya Kiafrika katika unyago wa chiputu una dhima,miongoni mwa dhima hizo ni kurithisha imani mbalimbali kwa kizazi kipya; kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana; kuifanya jamii ya Wamakonde kufanana na jamii nyingine za Kiafrika; kuendeleza umoja, amani na utangamano katika jamii ya Wamakonde, na; kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika jamii ya Wamakonde. Hata hivyo, inapendekezwa kufanyika kwa tafiti zaidikuhusu usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika vipengele vingine vya unyago kama vile hadithi, maigizo na misemo, ili kuweza kutoa majumuisho kuhusu usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika unyago wa Wamakonde. Aidha, tafiti zaidi zinahitajika ili kulinganisha usawiri wa falsafa ya Kiafrika katika nyimbo za unyago wa jamii ya Wamakonde na unyago wa jamii nyingine.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8482.M8K37)

Keywords

Makonde language, Makonde (African people), Nyimbo za unyago, Chiputu

Citation

Katoto, Z. J. (2016). Usawiri wa falsafa ya kiafrika katika unyago wa jamii ya wamakonde: uchunguzi wa nyimbo za unyago wa Chiputu. Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.