Matumizi ya mafumbo na taswira katika nyimbo za mapenzi za taarab asilia ya zanzibar
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Lengo la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya mafumbo na taswira katika nyimbo za mapenzi za taarab asilia ya Zanzibar. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Semiotiki. Nadharia hii ilimsaidia mtafiti katika uchambuzi wa data kwa kupitia misimbo ya kihemenitiki, matukio, kiseme, kirejelezi na kiishara. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni kufanya mahojiano ya ana kwa ana na watafitiwa, hojaji na ushuhudiaji wa maonesho ya muziki wa taarab. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa nyimbo za muziki wa taarab asilia ya Zanzibar zina matumizi makubwa ya mafumbo na taswira. Ingawa baadhi ya nyimbo hizo zilikuwa ni za matusi, lakini matusi hayo yaliweza kusawiriwa kwa lugha ya picha na mafumbo ambayo yaliweza kujenga taswira tofauti kulingana na ufahamu wa msikilizaji. Matumizi hayo ya taswira na mafumbo yana dhima mbalimbali kama vile kuonya na kuadilisha, kuficha matusi na karaha, kuepusha ugomvi na mafarakano, kuchemsha bongo, kuleta ujumi wa kisanaa na kufikisha ujumbe ipasavyo. Hivyo, utafiti huu umetoa ushauri kwa wasanii na watribu wa muziki huu wa taarab kuendelea kutunga nyimbo kwa lugha ya mafumbo na picha ili kudumisha utamaduni na maadili ya Wazanzibari.