Ujitokezaji wa Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya ya Kiswahili; uchaguzi wa adili na nduguze (1952) na siku ya watenzi wote (1968).
Loading...
Date
2019
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza ujitokezaji wa falsafa ya Ubuntu katika riwaya ya (1952) na Siku ya Watenzi Kiswahili ukijikita katika riwaya ya Adili na Nduguze Wale (1968). Utafiti huu uliongozwa na lengo kuu na malengo mahususi. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza ujitokezaji wa falsafa ya Ubuntu katika riwaya za Adili na Nduguze (1952) na Siku ya Walenzi Wow (1968) za Shaaban Robert.Malengo mahususi yalikuwa matatu nayo ni kubainisha vipengele vya falsafa ya Ubuntu vinavyojitokeza katika riwaya teule za Shaaban Robert, kueleza mbinu anuwai zinazotumika kusawiri vipengele hivyo vya Ubuntu na kufafanua umuhimu wa falsafa ya Ubuntu kisiasa katika riwaya hizo. Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu iliyoasisiwa na Tempels (1959) pamoja na wataalamu wengine ndiyo iliyotumika kutikia malengo ya utafiti huu. Ontolojia ya Kibantu ni mtazamo wa jamii ya Wabantu kuhusu maisha, kuwapo kwa mwanadamu na ulimwengu kwa ujumla. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani, mbinu za ukusanyaji wa data maktabani ulifanywa kwa kusoma maandiko na machapisho mbalimbali kwenye magazeti, majarida, vitabu vinavyohusiana na mada husika, pamoja na makala zilizo mtandaoni. Mtafiti alikusanya data zinazohusiana na falsafa ya Ubuntu kutoka katika riwaya zilizoteuliwa na kuzifafanua, kisha kubaini mbinu zilizotumika kusawiri falsafa ya Ubuntu katika riwaya hizo na umuhimu wa falsafa hiyo kisiasa. Tasinifu mbalimbali zilizozungumzia falsafa ya Ubuntu kwa namna mbalimbali zilitumika kupata taarifa. Vipengele vilivyojitokeza ndivyo vilivyojenga data kuu iliyofanyiwa uchambuzi na uhakiki. Matokeo ya data katika uchambuzi yalibainisha kwamba vipengele vya falsafa ya Ubuntu vinavyojitokeza katika riwaya hizo ni: utu, kazi, wema, busara, hekima na haki na usawa. Vipengele vingine ni ndoa, ukarimu, upendo, malezi, huruma halikadhalika umoja na ushirikiano. Mbinu mbalimbali zilizotumika kusawiri vipengele hivyo ni methali, barua, nyimbo, kilio, kicheko na lugha ya watoto. Ilibainika kwamba vipengele vya falsafa ya Ubuntu vina umuhimu mkubwa kisiasa katika riwaya teule. Umuhimu huo ni pamoja na kujenga uongozi bora, kusaidia raia wenye shida, kupigania haki na usawa, kujali utu wa raia, na kuwa mwema kwa raia. Aidha, utafiti umebaini kuwa mwandishi Shaaban Robert katika riwaya zake zilizotafitiwa amesawiri vipengele mbalimbali vya falsafa ya Ubuntu ambavyo tunaamini ndiyo falsafa iliyomkuza pamoja na jamii yake. Hii inatueleimisha zaidi kuhusu falsafa ya Shaaban Robert kuwa hakuathiriwa to na falsafa ya Kimagharibi na mtazamo wa dini ya Kiislamu. Utafiti huu umetoa muongozo kwa waandishi na wahakiki wa kazi za fasihi kuhusu ujitokezaji wa falsafa ya Ubuntu na inavyosawiri maisha ya waandishi na jamii kwa ujumla.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL 8703.5T34K29)
Keywords
Swahili literature, Ubuntu (philosophy), Fiction, Adili na nduguze (1952), Siku ya watenzi wote
Citation
Kavishe, Agricola Roman (2019) Ujitokezaji wa Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya ya Kiswahili; uchaguzi wa adili na nduguze (1952) na siku ya watenzi wote (1968).Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.