Usawiri wa mwanamke katika misemo iliyoandikwa katika vipepeo.

No Thumbnail Available
Date
2014
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Misemo ni fungu la maneno linalotumika ili kuleta maana na mafunzo fulani kwa jamii. Ni kipera kimojawapo kati ya vipera vya semi. Utafiti huu umechunguza usawiri wa mwanamke katika misemo iliyoandikwa katika vipepeo. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza usawiri wa mwanamke katika misemo ya vipepeo, kubainisha sababu za usawiri huo na kujadili athari za usawiri huo kwa jamii. Mbinu za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni ushuhudiaji, mahojiano na kupitia nyaraka maktabani, makavazi na katika tovuti. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data ni shajara na kalamu, simu ya mkononi, kamera na kompyuta. Nadharia ya unisai wa Kiafrika ndiyo iliyotumika kuchambua data za utafiti huu. Nadharia ya unisai wa Kiafrika ilitumika kwa sababu mwanamke aliyeangaliwa ni wa pwani ya Afrika Mashariki hivyo ilichaguliwa nadharia ambayo inachunguza taswira ya mwanamke katika fasihi ya Kiafrika. Kwa kiasi kikubwa matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti hivyo kukamilisha malengo ya utafiti kwani yalibaini kuwa mwanamke katika misemo ya vipepeo anasawiriwa katika namna hasi na chanya. Kwa upande wa usawiri hasi mwanamke anasawiriwa kuwa ni kiumbe duni na tegemezi, ni pambo la nyumba na ni chombo cha starehe. Upande wa usawiri chanya mwanamke anaonekana kuwa ni mwenye mapenzi ya dhati, ana msimamo katika mapenzi, ni mvumilivu na ni mzalishaji mali. Sababu za mwanamke kusawiriwa hivyo zinatokana na masuala ya dini, utamaduni, wanawake wenyewe kutopendana na kushirikiana na kukosa elimu kuhusu masuala ya jinsia. Athari za usawiri huo ni pamoja na mwanamke kuendelea kuwa katika nafasi ya unyonge, kutumia muda mwingi kujipamba, kujenga chuki miongoni mwa wanawake, na mwanamke kuwa na mwamko wa kujikomboa.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.M536)
Keywords
Proverbs, swahili, Swahili, Women
Citation
Mkomwa, A (2014) Usawiri wa mwanamke katika misemo iliyoandikwa katika vipepeo.Master dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.