Mabadiliko katika majigambo: uchunguzi wa majigambo ya jadi na ya bongo fleva
No Thumbnail Available
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia Mabadiliko katika Majigambo: Uchunguzi wa Majigambo ya Jadi na ya Bongo Fleva. Tulifanya utafiti ili kuhakiki madai kwamba tanzu mpya za fasihi zinazoibuka hujengwa katika misingi ya tanzu za awali. Majigambo ya jadi ni utanzu wa fasihi simulizi uliokuwapo tangu awali, majigambo yanayojitokeza katika muziki wa Bongo Fleva ni utanzu mpya; utafiti huu, kwa hiyo, umechunguza jinsi tanzu hizo mbili zinavyohusiana ili kuona kama majigambo ya Bongo Fleva yamechimbuka kutoka katika majigambo ya jadi. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha nduni za ushairi wa majigambo ya jadi na ya Bongo Fleva; kuzilinganisha na kuzilinganua nduni hizo; kueleza sababu za mabadiliko ya majigambo, na kueleza mchango wa mabadiliko hayo katika maendeleo ya fasihi simulizi. Ili kufikia malengo hayo, utafiti huu umetumia mbinu tano ambazo ni ukusanyaji wa matini, usikilizaji wa kanda na sidii, ushuhudiaji, usaili/mahojiano na utumiaji wa dodoso. Nazo nadharia zilizotumika ni nadharia ya Umbuji, na hasa Umbuji wa Daniel Kunene, Semiotiki na nadharia ya Ubadilikaji Mpya. Kuhusu matokeo, imebainika kwamba ushairi wa majigambo ya jadi na ule wa Bongo Fleva unafanana sana kimaudhui na kifani hivyo kuthibitisha kwamba majigambo ya Bongo Fleva yanachimbuka katika majigambo ya jadi. Ingawa kuna kufanana kwingi, aina hizo mbili za majigambo zina tofauti za namna fulani. Tofauti hizo ndogondogo zinazoonekana baina ya aina hizo mbili za majigambo, zinathibitisha kwamba ushairi wa majigambo unabadilika sambamba na mabadiliko yanayotokea katika jamii.
Description
Available in print form
Keywords
Fork literature, Swahili, Poetry, Swahili
Citation
Samwel, M (2012) Mabadiliko katika majigambo: uchunguzi wa majigambo ya jadi na ya bongo fleva, PhD (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.(Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)