Athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya kisiha

dc.contributor.authorKileo, Joan Godwin
dc.date.accessioned2020-04-07T14:28:27Z
dc.date.available2020-04-07T14:28:27Z
dc.date.issued2017
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8110.C595K54)en_US
dc.description.abstractLengo la utafiti huu ni kuchunguza athari za Kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha. Utafiti huu una malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha maneno ya lugha ya Kiswahili yaliyomo katika lugha ya Kisiha, kueleza athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha, na kufafanua sababu za athari za kimofofonolojia za lugha ya Kiswahili katika lugha ya Kisiha. Chanzo cha data kilichotumika katika utafiti huu ni uwandani. Data zilikusanywa kwa njia ya mahojiano, hojaji na ushuhudiaji kutoka kwa wazee wenye rika la kati ya miaka 50-85 na wanafunzi wa kati ya miaka 10-14 katika wilaya ya Siha. Data zilizopatikana katika utafiti huu zilichambuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles (1982). Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa lugha ya Kisiha imeathiriwa na lugha ya Kiswahili hasa katika kipengele cha mofolojia. Aidha, athari za kifonolojia zimejitokeza katika kipengele cha sauti za Kiswahili zilizotumiwa na watoa taarifa wakati walipokuwa wanazungumza Kisiha. Athari hizo ni matumizi ya sauti [z] badala ya sauti [s], sauti [m] badala ya sauti [n], sauti [ch] badala ya sauti [sh] pamoja na udondoshaji wa sauti [h] ya Kisiha. Fauka ya hayo, utafiti huu umeweka bayana sababu za athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha, ambapo miongoni mwa sababu hizo ni elimu, biashara, pamoja na upanuzi wa matumizi ya Kiswahili vijijni. Mwisho ni muhtasari wa utafiti, matokeo ya utafiti, mchango wa utafiti pamoja na mapendekezo ya tafiti fuatishi ambapo imependekezwa kuwa tafiti zifanyike katika vipengele ambavyo havikushughulikiwa, kama vile sintaksia na semantiki. Aidha, kuna haja ya kufanya tafiti kuhusu mbinu na mikakati ya kuchochea matumizi ya lugha ya Kisiha katika muktadha huu wa kutamalaki kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kudumisha lugha ya Kisiha.en_US
dc.identifier.citationKileo, J.G. (2017) Athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya kisiha. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9158
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSiha languageen_US
dc.subjectChaga languageen_US
dc.subjectPhonologyen_US
dc.titleAthari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya kisihaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Joan Godwin Kileo.pdf
Size:
179.12 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: