Muundo wa Vishazi Tegemezi-Bebwa Katika Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiri huu unahusu Muundo wa Vishazi Tegemezi-bebwa Katia Kiswahili kwa kutumia Nadharia ya Sarufi Geuza Maumbo Zalishi. Utafiti huu ulifanyika katika vhuo kikuu cha dar es salaam, Kampusi Kuu Ya Mwalimu J.K. Nyerere pamoja na chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam. Data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu za hojaji,mahojiano, kushiriki na usomaji matini.Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili ina vishashi tegemezi-bebwa angalau vine, yaani kishazi rejeshi,kishazi nomino, kishazi shirikishi na kishazi kitenzi kisicho-ukomo.Muundo na mwenendo wa vishazi hivi hutofautiana kwa namna mpja au nyingine. Utafii huu umeonesha kuwa vishazi tegemezi-bebwa vya urejeshi na ushirikishi hufungamana na KN kwa njia ya ukumushi wakati kishazi nomino na kitenzi kisicho-ukomo hufungamana na KT kwa njia ya ujazilizi. Utafiti umeonesha masharti na mazingira ya utokeaji wa kila kishazi. Vilevile utafitiumeeleza kanuni na michakato ya kimageuzi katika uundaji wa kila KSTB. Kanuni hzo ni pamoja na udondoshaji, uhamishaji, uchopekaji, ubadala,ubadilishanaji nafasi pamoja na upatanisho wa lisarufi. Imependekezwa kuwa tafiti zaidi zifanyike kuhusu vipengele vingine vinavyoandamana na vishazi tegemezi si bebwa. Pia inapendekezwa kufanyika Kwa tafiti linganishi kati ya KSTB vya Kiswahili na lugha nyingine. Kadhalika ufanyike utfiti kwa kila KSTBna si kuvijumuisha Kama utafiti huu uliofanya.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702.E38)
Keywords
Swahili language, Grammer
Citation
Edward, Samson (2016) Muundo wa Vishazi Tegemezi-Bebwa Katika Kiswahili, Master dissertation, University of Dar es Salaam