Tofauti za kimsamiati katika lahaja za Kinyaturu

No Thumbnail Available
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Suala la utofauti wa kimsamiati katika lahaja mbalimbali limewavuta wataalamu wengi. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanyika katika lugha ya Kinyaturu. Utafiti huu ulikuwa jaribio la kuchunguza utofauti wa kimsamiati katika lugha hii na kubainisha tofauti hizo za kimsamiati na sababu za kuwepo kwa utofauti huo. Utafiti umefanyika katika vijiji vya Ng’ongoampoku na Mtimko katika Wilaya ya Singida, Tanzania. Mbinu za utafiti zilihusu: usampulishaji, ukusanyaji wa data uwandani, uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Data ya utafiti ni ya kutoka uwandani ambapo misamiati mbalimbali ya Kiswahili iliteuliwa ili watafitiwa waingize tafsiri katika lahaja zao husika.Kazi imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza, imeeleza kiini cha utafiti na utaratibu uliozingatiwa katika kufanikisha utafiti. Sura ya pili, imeshughulikia mapitio ya maandiko kuhusiana na maandiko yanayohusu lahaja mbalimbali zilizowahi kuandikiwa. Sura ya tatu, imehusu mbinu za utafiti ambapo populesheni, sampuli, usampulishaji pamoja na njia mbalimbali za ukusanyaji data zilibainishwa. Sura ya nne, imeshughulikia uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Data iliyokusanywa imechanganuliwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Nadharia ya Makutano na Mwachano iliongozo mjadala na uchanganuzi wa data hii. Sura ya tano imeshughulikia matokeo, hitimisho, na tafiti fuatishi. Matokeo ya utafiti yamebainisha utofauti wa msamiati unaojitokeza katika lahaja za Kinyaturu na sababu za kuwepo kwa utofauti huo.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025.T34W44)
Keywords
Nyaturu language, Nyaturu (African people)
Citation
Wilson, A (2013) Tofauti za kimsamiati katika lahaja za Kinyaturu.Master dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.