Misemo ya kiswahili katika vazi la fulana: uchambuzi wa dhamira na matumizi ya lugha

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu misemo ya Kiswahili iliyoandikwa katika vazi la fulana. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza dhamira radidi zilizojitokeza katika misemo ya Kiswahili iliyoandikwa katika fulana, kuchambua vipengele mbalimbali vya lugha vilivyojitokeza katika misemo hiyo, pamoja na kujadili dhima ya misemo hiyo kwa fasihi na kwa jamii. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya tatu, yaani Temeke, Kinondoni na Ilala. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Sosholojia na nadharia ya Semiotiki. Watafitiwa 34 walihojiwa katika utafiti huu, ambapo njia ya sampuli nasibu na sampuli lengwa zilitumika kuwapata watafitiwa hao kwa kuzingatia kigezo cha umri na jinsia. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data katika kazi hii ni ushuhudiaji, mahojiano pamoja na kupitia kazi za maktabani, makavazi na tovuti. Matokeo ya utafiti yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha dhamira mbalimbali kama vile maradhi ya UKIMWI, umaskini, dini, chuki na wivu, elimu, maisha na umuhimu wa kufanya kazi. Utafiti huu pia ulibaini vipengele mbalimbali vya lugha vilivyopo katika maandishi kwenye fulana kama vile lugha ya tamathali za usemi, misimu na lugha ya mitaani, majigambo, pamoja na mitindo ya lugha kama vile kuchanganya herufi na namba, na kuchanganya lugha mbili katika msemo mmoja. Pia, matokeo hayo yalibainisha kuwa misemo hii imeweza kuleta mchango mkubwa kwa jamii na kwa fasihi katika kuhifadhi na kukuza lugha, kukuza ubunifu, kuelimisha, kuonya, kukosoa, kuhimiza kufanya kazi na kuburudisha.
Description
Keywords
Swahili language, Proverbs, Swahili
Citation
Rajabu, A (2012) Misemo ya kiswahili katika vazi la fulana: uchambuzi wa dhamira na matumizi ya lugha, Tasinifu ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatika http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)