Uchambuzi wa maana na dhima za sitiari katika maandishi ya bajaji

Date

2019

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu ulilenga kuchunguza maana na dhima za sitiari zitokeazo kwenye maandishi ya bajajini. Utafiti huu umefanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya za Kinondoni na Ubungo. Katika wilaya ya Kinondoni utafiti ulifanyika katika kata za Kinondoni na Kawe: na katika Wilaya ya Ubungo, utafiti ulifanyika katika kata ya Ubungo. Mbinu za utafiti zilihusisha uteuzi wa sampuli na usampulishaji, mbinu za ukusanyaji data na mbinu za uchambuzi wa data. Data ya utafiti iliyohusika katika utafiti huu ni maandishi yaliyoandikwa kwenye bajaji yaliyokusanywa na mtafiti kutoka uwandani. Watafitiwa walisailiwa ili kupata dhima ya sitiari zilizobainishwa. Utafiti huu pia ulitumia data za maktabani, zinazohusu sitiari. Kazi hii imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imetoa maelezo ya kiini cha tatizo na mbinu ambazo zimetumika katika kufikia mahitimisho. Sura ya tatu imezungumzia na kujadili mbinu mbalimbali za utafiti ambazo ni sampuli na usambulishaji, mbinu za kukusanya data na mbinu zilizotumika kuchanganua data. Sura ya nne imeshughulikia uwasilishaji na uchanganuzi wa data. Data za uwandani zimechanganuliwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Uchanganuzi huu wa data umeongozwa na “Nadharia ya Maana kama Matumizi. “Nadharia hii imeasisiwa na mwanafalsafa Wittgenstein (1953). Msingi wake mkuu umejikita katika kusistiza kuwa “maana ya neno iko katika matumizi yake.” Na lugha hufungamanishwa na tabia za binadamu na namna wanavyohusiana baina yao. Kwa jumla, matumizi”. Sura ya tano imeshughulikia matokeo ya utafiti, hitimisho na mapendekezo ya utafiti fuatishi. Matokeo ya utafiti yambainisha kuwa maana za sitiari hupatikana kwa kuzingatia muktadha unaohusika. Huwezi kupata maana bila kujua sababu, lengo na makusudio ya sitiari hiyo. Maana inayohamishwa hutegemea muktadha unaohusisha tukio. Vilevile, lengo kubwa la dhima zilizopatikana katika sitiari hizo ni kuwaasa na kuwakumbusha wanadamu jinsi ya kuishi katika jamii. Kutokana na matokeo hayo tunajifunza kuwa huwezi kupata maana nje ya muktadha unaohusika. Utafiti pia unapendekeza kuwa huwezi kupata maana nje ya muktadha unaohusika. Utafiti pia unapendekeza kuwa tafiti fuatizi zifanyike kuhusu (a) kutotumika sana kwa sitiari katika maandishi ya bajaji, na (b) uhusiano baina ya maana na dhima za sitiari.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8703.5.K3965)

Keywords

Swahili literature, Swahili drama, Magic in Literature, Emmanuel Mbogo, Ngoma ya ng`wanamalundi, Sundiata

Citation

Stephen, S. (2019). Uchambuzi wa maana na dhima za sitiari katika maandishi ya bajaji. M.A Kiswahili. University of Dar es Salaam. Dar es Salaam