Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na kindali Hassan Musa Tasnifu ya (Kiswahili) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi Ya Taaluma ya Kiswahili, 2019 Lugha ina miundo mbalimbali, miundo mingine ina upekee na umuhimu fulan. Kwa hiyo, miundo hiyo huvuta udadisi haraka. Moja ya miundo hiyo ni vishazi rejeshi ambavyo vina mwigo mpana katika lugha za kibantu kwa vile vishazi hivi ndivyo vyenye kutumika mara nyingi zaidi kukumusha nomino. Vivumishi katika lugha za kibantu ni vichache kwa vile kazi za vivumishi hufanywa na vishazi rejeshi, kwa hiyo, urejeshi ni muundo muhimu katika lugha hizi. Utafiti huu unahusu “Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na Kindali” utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Sarufi Geuzi ya Chomsky (1965) utafiti huu ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika mkoa wa Dar es salaam na Bundali katika wilaya ya Ileje Mkoani Songwe. Data ya utafiti huu ilikusanywa maktabani na uwandani kwa njia ya hojaji, mahojiano na kusoma na kuchambua matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba vishazi rejeshi katika Kiswahili na kindali vinafanana katika matumizi na kutofautiana katika baadhi ya miundo. Muundo wa kishazi rejeshi unatofautiana katika lugha hizi katika idadi ya miundo na mumbo la kiwakilishi rejeshi. Kiswahili kina miundo mitatu wakati kindali kina muundo mmoja wa kishazi rejeshi kwa kuzingatia kiwakilishi rejeshi kinapachikwa wapi. Hata hivyo, kiwakilishi rejeshi katika kiwahili ni mofimu tegemezi wakati katika Kindali kiwakilishi rejeshi ni mofimu huru. Muundo wa Kishazi rejeshi kutokea baada ya neno kuu kutangulia unafanana katika lugha hizi. Vilevile matumizi ya kishazi rejeshi katika lugha hizo yanafanana katika ukumushi bainifu, ukumushi ziada na uelezi wa namna na mahali. Utafiti huu umeonesha masharti na michakato ambayo kishazi rejeshi hupitia katika uundaji wake. Masharti hayo ni kuwepo kwa vishazi huru viwili vyenye uzito sawa, vishazi hivyo sharti niwe na nomino zenye kurejelea kitu kilekile na sharti la tatu ni kukishusha hadhi kishazi huru kimoja. Sharti la kushusha hadhi kishazi huru kimoja linafungamana na michakato ya udondoshaji, uwakilishi na urejeshi, uchopekaji, utegemezaji, uhamishaji na kubadilishana nafasi. Maeneo mengine yanayopendekezwa kufanyiwa utafiti ni katika aina zingine za vishazi tegemezi.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Abstract

Description
Available in print form, East Africana collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8025.1 M972)
Keywords
African language,, Bantu language,, Swahilli Language,, Grammar,, Ndali language
Citation
Musa, H(2019)Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na kindali Hassan Musa Tasnifu ya (Kiswahili) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi Ya Taaluma ya Kiswahili, 2019 Lugha ina miundo mbalimbali, miundo mingine ina upekee na umuhimu fulan. Kwa hiyo, miundo hiyo huvuta udadisi haraka. Moja ya miundo hiyo ni vishazi rejeshi ambavyo vina mwigo mpana katika lugha za kibantu kwa vile vishazi hivi ndivyo vyenye kutumika mara nyingi zaidi kukumusha nomino. Vivumishi katika lugha za kibantu ni vichache kwa vile kazi za vivumishi hufanywa na vishazi rejeshi, kwa hiyo, urejeshi ni muundo muhimu katika lugha hizi. Utafiti huu unahusu “Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na Kindali” utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Sarufi Geuzi ya Chomsky (1965) utafiti huu ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika mkoa wa Dar es salaam na Bundali katika wilaya ya Ileje Mkoani Songwe. Data ya utafiti huu ilikusanywa maktabani na uwandani kwa njia ya hojaji, mahojiano na kusoma na kuchambua matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba vishazi rejeshi katika Kiswahili na kindali vinafanana katika matumizi na kutofautiana katika baadhi ya miundo. Muundo wa kishazi rejeshi unatofautiana katika lugha hizi katika idadi ya miundo na mumbo la kiwakilishi rejeshi. Kiswahili kina miundo mitatu wakati kindali kina muundo mmoja wa kishazi rejeshi kwa kuzingatia kiwakilishi rejeshi kinapachikwa wapi. Hata hivyo, kiwakilishi rejeshi katika kiwahili ni mofimu tegemezi wakati katika Kindali kiwakilishi rejeshi ni mofimu huru. Muundo wa Kishazi rejeshi kutokea baada ya neno kuu kutangulia unafanana katika lugha hizi. Vilevile matumizi ya kishazi rejeshi katika lugha hizo yanafanana katika ukumushi bainifu, ukumushi ziada na uelezi wa namna na mahali. Utafiti huu umeonesha masharti na michakato ambayo kishazi rejeshi hupitia katika uundaji wake. Masharti hayo ni kuwepo kwa vishazi huru viwili vyenye uzito sawa, vishazi hivyo sharti niwe na nomino zenye kurejelea kitu kilekile na sharti la tatu ni kukishusha hadhi kishazi huru kimoja. Sharti la kushusha hadhi kishazi huru kimoja linafungamana na michakato ya udondoshaji, uwakilishi na urejeshi, uchopekaji, utegemezaji, uhamishaji na kubadilishana nafasi. Maeneo mengine yanayopendekezwa kufanyiwa utafiti ni katika aina zingine za vishazi tegemezi,Masters Dissertation,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dar es salaam.