Utani wa jadi baina ya timu ya Simba na Yanga: uchunguzi wa lugha na athari zake.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu utani wa jadi wa timu ya Simba na Yanga. Malengo mahususi yaliyoongoza utafiti huu ni pamoja na kufafanua miktadha ya utendaji wa utani, kubainisha vipengele vya lugha vinavyotumia utani na mwisho ni kujadili athari ya lugha hiyo ya utani kifasihi na kijamii. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya tatu, ambazo ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Mbinu zilizotumika katika kukusanya data za utafiti huu ni udurusu wa machapisho maktabani, ushuhudiaji na mahojiano. Njia ya sampuli lengwa na sampuli nasibu zilitumika ili kuwapata watafitiwa kwa kuzingatia kigezo cha umri na jinsia. Makundi hayo ya watafitiwa ni viongozi, wafanyakazi, mashabiki na wachezaji wa zamani. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Sosholojia na Nadharia ya Semiotiki. Matokeo ya utafiti yamebaini miktadha ya utendaji wa utani ni nje ya uwanja, ndani ya uwanja na kupitia usajili wa wachezaji. Utafiti huu pia umebainisha vipengele mbali mbali vya lugha vinavyotumia utani kama tamathali za usemi (sitiari, dhihaka na vijembe), matumizi ya lugha ya majigambo na matumizi ya misimu. Vilevile matokeo ya utafiti huu yameonyesha athari ya lugha ya utani kifasihi na kijamii. Miongoni mwa athari zenye tija ni pamoja na kuimarisha timu na kuzipa umaarufu, kuvutia mashabiki kwenda uwanjani, kujenga umoja na ushirikiano, kuhifadhi, kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, kuelimisha na kuonya jamii, kuburudisha jamii na kuhifadhi mila. Madhara ya utani ni pamoja na kusababisha ugomvi, kuvunjiana heshima, kujenga hofu kwa timu pinzani na kusababisha vifo.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.M8521)
Keywords
Folk literature, Swahili langauge, Tanzania
Citation
Mwagike, A. E. (2016). Utani wa jadi baina ya timu ya Simba na Yanga: uchunguzi wa lugha na athari zake. Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.