Upanuzi wa maana za maneno katika mazungumzo ya Kiswahili: mifano kutoka vitenzi vya Kiswahili.

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu upanuzi wa maana za maneno katika mazungumzo ya Kiswahili. Jumla ya vitenzi 40 vimechunguzwa katika utafiti huu. Eneo ambalo utafiti huu umefanyika ni katika kata za Ubungo, Mbezi na Manzese zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Vijana ndio waliohusishwa katika kutoa taarifa zinazohusiana na mada ya utafiti huu. Data ya utafiti huu imepatikana kwa kutumia mbinu tatu; yaani hojaji, mahojiano na Maktabani. Data iliyokusanywa imechambuliwa kwa kutumia nadharia ya Umaanilizi wa Mazungumzo ya Herbert Paul Grice (1975). Hata hivyo, uchambuzi wa data umefanyika kwa kutumia mikabala miwili, mkabala wa kimaelezo na mkabala wa kiidadi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa pamoja na maneno kuwa na maana zake za msingi, bado maana hizo hupanuliwa katika mazungumzo hali ambayo husababisha kuongezeka kwa maana za ziada katika maneno ya lugha. Pia, imebainika kuwa maana za kingono zinaongezeka kwa kasi katika maneno ya lugha kutokana na upanuzi unaofanywa katika mazungumzo ya Kiswahili. Vilevile, imebainika kuwa katika mazungumzo, mzungumzaji na msikilizaji wote wanahusika katika kupanua maana za maneno. Kutokana na kuibuka kwa maana nyingine kuendelea kutokea katika maneno ya lugha, utafiti huu unapendekeza kuwa maana zinazodumu ziingizwe katika kamusi ili watumiaji wa lugha waweze kuzirejelea pindi inapobidi kuzirejelea. Pia, kwa kufanya hivyo, itawasaidia hata wajifunzaji wa Kiswahili kama lugha yao ya pili kung’amua maana kama hizo katika muktadha unaohusika. Aidha, tafiti nyingine zinaweza kuchunguza upanuzi wa maana za maneno katika aina nyingine za maneno kwa kuwa mabadiliko ya maana ni suala endelevu.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.E44)

Keywords

Swahili language, Dictionaries

Citation

Elias, S. (2016). Upanuzi wa maana za maneno katika mazungumzo ya Kiswahili: mifano kutoka vitenzi vya Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.