Mfumo wa uwakilishi wa nafsi katika vitenzi vya kiswahili cha Pemba
No Thumbnail Available
Date
2015
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia Mfumo wa Uwakilishi wa Nafsi katika Vitenzi vya Kiswahili cha pemba . Utafiti umefanyika katika kitongoji cha Kiuyu wilaya ya Wete na Konde wilaya ya Micheweni katika mkoa wa Kaskazini Pemba. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya maktabani pamoja na mbinu ya uwandani. Katika mbinu ya uwandani utafiti umetumia njia ya hojaji, majadiliano na ushuhudiaji katika ukusanyaji wa data. Data zilizopatikana katika utafiti huu zimechambuliwa kwa mkabala usio wa kiidadi (mkabala wa kimaelezo), hata hivyo majedwali yametumika ili kumrahisishia msomaji kuelewa kwa wepesi. Ili kufanikisha utafiti huu nadhari ya Mofolojia Leksika (ML) ya Kiparsky (1982) imetumika katika uwasilishaji na uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba kiasi kikubwa maumbo yanayowakilisha nafsi katika Kipemba huathiriwa na michakato mbalimbali ya kifonolojia na kimofolojia ikiwemo udondoshaji na uyeyushaji ambayo husababisha baadhi ya vitamkwa kudondoshwa au kubadilishwa kwa mujibu wa mazingira ambayo viambishi hivyo vinakuwepo. Aidha, matokeo yanaonesha kuwa viwakilishi nafsi katika vitenzi vya Kipemba hubadilika kwa mujibu wa mabadiliko ya kitenzi katika hali na nyakati mbalimbali Kwa upande wa uamilifu, matokeo yanaonesha kwamba, baadhi ya viwakilishi nafsi katika vitenzi vya Kipemba hufanya kazi ya kuwakilisha nafsi pamoja na dhana nyingine kama vile njeo, ilhali baadhi hufanya kazi ya kuwakilisha nafsi pekee. Ingawa utafiti huu umechambua mfumo wa uwakilishi wa nafsi katika vitenzi vya Kipemba, bado kuna haja ya uchunguzi na uchambuzi wa kina zaidi juu ya unyambulishaji wa vitenzi vya Kipemba kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na kuangalia kufanana na kutofautiana kwake na Kiswahili Sanifu.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.Z9A22)
Keywords
Swahili language, Dialects, Pemba Island, Tanzania
Citation
Abass, Z. M. (2015) Mfumo wa uwakilishi wa nafsi katika vitenzi vya kiswahili cha Pemba, Master dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam