Maudhui katika nyimbo za taarab za bi Shakila

dc.contributor.authorMzee, Fatma Aboud
dc.date.accessioned2020-04-28T21:21:03Z
dc.date.available2020-04-28T21:21:03Z
dc.date.issued2013
dc.descriptionAvailable in printed form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.S24M93)en_US
dc.description.abstractLengo la utafiti huu ni kuchunguza nafasi ya maudhui katika nyimbo za taarab za Bi. Shakila yanavyosawiri hali halisi ya jamii. Utafiti huu ulipitia machapisho mbalimbali na data za msingi zilipatikana kwa kufanya usaili na msanii teule Bi. Shakila pamoja na watafitiwa wengine. Data za upili zilipatikana katika maktaba, makumbusho na kwenye mtandao. Nadharia ya semiotiki kupitia misimbo yake kama kihementiki, ishara, kirejelezi, matukio na kiseme ndio iliyosaidia uchambuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa nyimbo za Bi. Shakila zimeshamiri dhamira kadha wa kadha. Baadhi yake ni umalaya, ufisadi, umbeya, mmomonyoko wa maadili, dini, malezi bora, umuhimu wa tabia njema, umuhimu wa wazazi, ukombozi, matendo mema, umuhimu wa kuilinda nchi na umuhimu wa mapenzi. Dhamira ambazo zinasawiri maisha halisi ya mwanadamu katika jamii yetu. Matokeo ya utafiti huu pia yamebaini kuwa nyimbo za Bi. Shakila zimetumia matumizi mbalimbali ya lugha ili kufikisha maudhui yaliyokusudiwa kwa hadhira. Hii ni pamoja na kuficha lugha ya matusi ili kuondoa karaha, kuepusha ugomvi na mfarakano miongoni mwa jamii. Matumizi hayo ya lugha ni pamoja na taswira na ishara, tamathali za semi, methali na mafumbo. Hivyo, utafiti huu unatoa maoni kwa watunzi wa nyimbo za taarab kutunga nyimbo ambazo zinazingatia maadili, zinaelimisha, zinaonya na kurekebisha jamii. Maoni na mapendekezo pia yametolewa kwa serikali, watafiti na jamii kwa ujumla.en_US
dc.identifier.citationMzee, F. A (2013) Maudhui katika nyimbo za taarab za bi Shakila, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/10452
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectSaid, Shakilaen_US
dc.titleMaudhui katika nyimbo za taarab za bi Shakilaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Fatma Aboud Mzee.pdf
Size:
27.16 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: