Ulinganisho wa vikundi nomino vya Kiswahili na Kivunjo

Loading...
Thumbnail Image
Date
1976
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Madhumuni ya tasnifu hii ni kujaribu kulinganisha lugha mbili za Kibantu:- Kivunjo lugha ya kuzaliwa na Kiswahili lugha ya pili. Katika lugha hizi mbili, uchunguzi wake bado ni duni sana, kwa hiyo mengi yatakayojitokeza ni kutokana na juhudi za kibinafsi katika kutafuta na kupekuwa maandishi mbalimbali kuhusu lugha kwa ujumla nay ale machache yaliyowahi kuandikwa kuhusu Kiswahili na lugha nyingine za Kibantu. Mengine pia yametokana na watumiaji wa lugha hizi, mimi binafsi nikiwa mmojawapo. Watumiji wa lugha ya Kiswahili ni wakazi wa Tanzania na baadhi ya nchi za jirani. Niliohusu nao hapa ni watanzania tu. Watumiaji wa Kivunjo ni kikundi cha wachagga waishio kwenye miteremko yam lima Kilimanjaro katika wilaya ya Moshi, katikati ya wilaya za Hai na Rombo. Wenyewe hawakiiti Kivunjo, bali “Kianjo” kutokana na wakazi wake, Waanjo. Hawa ni watu waishio sehemu za Kirua, Kilema, Marangu, Mamba na Mwika. Wamochi wakaao sehemu ijulikanayo kama “Old Moshi” nao pia hutumia kilugha hiki ingawaje tofauti zilizopo kati ya watumiaji wa sehemu hizi nyingine. Tofauti hizo sitaziingilia katika tasnifu hii ila nitajishughulisha na Kivunjo kama watumiavyo Waanjo wa Kirua Vunjo – sehemu Kivunjo na Kiswahili. Hii itafanyika kama ifuatavyo. 1. Uchunguzi kuhusu ngeli za majina. Hapa dhana mbalimbali za wanaisimu zimejitokeza . Nadharia iliyotumika hasa ni ile ya upatanisho wa Kisarufi na utumiaji hasa ni ile ya upatanisho wa Kisarufi na utumiaji wa namba, kuainisha ngeli hizo. Vipengele vinginevyo vihusuvyo dhana ya ngeli pia vimejadiliwa. Matatizo yatajitokeza katika uchambuzi huu hasa katika Kivunjo ingawaje hayataelezwa kwa kirefu sana. 2. Uchambuzi wa vikundi nomino vyenyewe katika usawia wa vipashio muhimu K (Kisifio) Sh (Shina) na S (sifa).Sehemu hii ndio itakayokuwa muhimu kwa sababu inahusika zaidi katika tasnifu hii katika kivajadili vikundi nomino vya lugha hizi mbili: Nadharia ya “Scale and Categories of Grammar” ya Halliday (1961) ndio itakayotumika katika kujaribu kutekeleza lengo hili. Matatizo yatokanayo nayo yataelezwa pahitajipo. 3. Mahitimisho –sehemu hii itaonyesha marejeo ya kazi yote na kujaribu kuzilinganisha lugha hizi mbili: Muundo na mpangilio wa vikundi nomino ndiyo mambo yatakayo shughulikiwa katika ulinganisho huu, ulingano na tofati zikionyeshwa kwa maelezo mafupi iwezekanavyo. Kufaulu na kutofaulu ni sehemu ndogo pia itakayojitokeza hapa katika kuchambua vikundi nomino na vipashio vyake kwa kutumia nadharia itakayopendekezwa. Sababu zilizokuwa dhahiri zitatajwa, pasipowezekana, mapendekezo yatatolewa.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8003.T3M6)
Keywords
Lugha, Kiswahili na Kivunjo, Lugha ya Kivunjo, Tanzania
Citation
Moshi, L (1976) Ulinganisho wa vikundi nomino vya Kiswahili na Kivunjo, Tasnifu ya (M.A )Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dar es salaam,