Uangavu wa kimofosemantiki katika nomino na vitenzi vya kiswahili sanifu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulichunguza Uangavu wa Kimofosemantiki katika Nomino na Vitenzi vya Kiswahili Sanifu. Data ya utafiti huu ilipatikana kwa njia ya uchambuzi matini na hojaji. Kisha, ilichambuliwa kwa kuwekwa katika mafungu mbalimbali. Data iliyofanana iliwekwa katika fungu moja. Hivyo, kulikuwa na mafungu makuu matatu yaliyotokana na maswali ya utafiti. Kwa hiyo, data iliyojibu swali husika iliwekwa katika fungu moja. Pamoja na hayo, katika swali la kwanza, data iliwekwa katika mafungu mengine madogo ambapo yalipatikana mafungu makuu mawili: fungu la kwanza lilihusu nomino zenye uangavu wa kimofosemantiki wakati fungu la pili lilihusu vitenzi vyenye uangavu wa kimofosemantiki. Kisha, mkabala wa kitaamuli ulitumika katika kuielezea data hizo. Pia, utafiti huu ulitumia Nadhariatete ya ungavu wa kisemantiki iliyopendekezwa na Vennemann (1972). Msingi wa nadharia ulitumika kuonesha namna uangavu wa kimofosemantiki unavyotokea katika nomino na vitenzi vya Kiswahili Sanifu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa baadhi ya nomino na vitenzi vya Kiswahili Sanifu hupata uangavu wa kimofosemantiki. Uangavu huu hutokana na uhusiano wa maana ya vijenzi vya maneno hayo. Mwisho utafiti huu unapendekeza kuwa, utafiti kama huu unaweza kufanyika katika lahaja nyingine za Kiswahili kama vile Kitumbatu, Kivumba, Kimakunduchi na Kimvita kwa kutaja chache. Pamoja na kuwa lugha hizi zinatokana na mzizi mmoja lakini zinaweza zikawa tofauti katika baadhi ya sifa zake. Hivyo, zinapaswa zichunguzwe. Pia, kwa kuwa lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kibantu, utafiti kama huu unaweza kufanyika katika lugha nyingine za Kibantu kama vile Kimakonde, Kinyamwezi, Kihaya na Kichaga kwa kutaja chache.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702.H82)
Keywords
Swahili language, Semantics, Morphology, Noun
Citation
Hudson, R. R. (2016) Uangavu wa kimofosemantiki katika nomino na vitenzi vya kiswahili sanifu, Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Dar es Salaam, Dar es Salaam