Ubadilikaji msimbo na aina zake: Mifano kutoka katika shule za sekondari za kata katika wilaya ya Butiama.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Wakati lugha ya kufundishia katika shule za sekondari za kata ikiwa ni Kiingereza kulingana na sera ya elimu ya Tanzania, kumekuwa na utumiaji wa lugha zaidi ya moja katika mawasiliano ya walimu na wanafunzi ikihusisha lugha za Kingereza na Kiswahili na lugha mama za eneo ambapo shule hizo zipo. Kutokana na hali hiyo utafiti huu ulijikita katika kuchunguza ubadilikaji msimbo na aina zake kwa kuchukua mifano kutoka katika shule za sekondari za kata nchini Tanzania. Utafiti huu ulifanyika katika Wilaya ya Butiama katika shule za sekondari za kata za Butuguri, Bumangi, Buhemba, Butiama, Buruma, Mirwa na Mazami katika vipindi vya masomo ya Kingerezana Kiswahili. Utafiti huu umetumia nadharia ya model ya utambulisho (MU) yaani ‘’Markedness Model’’ ya scotton (1993), pia data zilikusanywa kwa kutumia njia ya ushuhudiaji, hojaji, usaili na kinasasauti. Katika kuchanganua data mtafiti ametumia mbinu za uchanganuzi wa data wa kimaelezo na kitakwimu kwa kuziweka data katika majedwali na katika makundi. Utafiti huu ulibaini kuwa mazungumzo ya walimu wenyewe, wanafunzi wenyewe na walimu na wanafunzi nje ya darasa yalibeba ubadilikaji Msimbo ndani. Mazungumzo yanayofanyika ndani ya darasa baina ya walimu na wanafunzi yalihusisha zaidi ubadilikaji Msimbo kati. Lugha zinazobadishwa zaidi katika mazungumzo ya walimu wenyewe, wanafunzi na walimu na wanafunzi wenyewe, hasa wa kidato cha nne, ni Kiswahili na Kiingereza, huku kidato cha kwanza wakibadili zaidi Kiswahili na Kizanaki. Vilevile, mitazamo ya walimu na wanafunzi kuhusu ubadilikaji msimbo katika mawasiliano imegawanyika katika kundi chanya na kundi hasi. Kundi chanya lilikuwa na mtazamo kwamba; ubadilikaji msimbo huondoa matabaka baina ya wazungumzaji, mbinu mbadala ya kusisitiza jambo, huwafurahisha wazungumzaji na wasikilizaji, nan i mbinu mojawapo ya kuongeza maarifa katika lugha. Pia husaidia kuleta maelewano baina ya wazungumzaji. Kundi hasi lilikuwa na mtazamo kwamba; ubadilikaji msimbo huleta utata katika utamaduni wa lugha husika, ni ukiukaji wa kanuni za lugha, utumiaji wa kizanaki katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza ni kutokana na kuathiriwa na lugha mama, hawapendezwi na utumiaji wa lugha zaidi ya moja katika mawasiliano na hauna umuhimu wowote. Kwa ujumla utokeaji wa ubadilikaji msimbo ni kawaida ambayo haiepukiki katika mawasiliano kama utafiti huu ulivyobaini na kwa hakika inapendezesha mazungumzo licha ya kuwa na athari hasi chache.
Description
Available in printed form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8701.K33)
Keywords
Swahili language, English language, Zanaki language, Butiama, Tanzania
Citation
Kagemro, A. (2013) Ubadilikaji msimbo na aina zake: Mifano kutoka katika shule za sekondari za kata katika wilaya ya Butiama. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.