Matatizo ya kiuhariri katika vitabu vya kiada vya Kiswahili nchini Tanzania

Loading...
Thumbnail Image
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu matatizo ya kiuhariri katika vitabu vya kiada vya Kiswahili nchini Tanzania. Katika utafiti huu tulijikita katika malengo mahususi matatu: Lengo la kwanza lilikuwa ni kubainisha makosa ya kiuhariri katika vitabu vya kiada vya shule za msingi. Pili, kueleza sababu za kuwapo kwa makosa hayo. Tatu, kupcndekeza mbinu za utatuzi wa makosa hayo. Kufanyika kwa utafiti huu kulichochewa na kuwapo kwa malalamiko mengi ya kiufundi katika tasnia ya uchapishaji, kwani baadhi ya tafiti zimeeleza kwa ufupi sana kero zinazojitokeza katika vitabu (Thonya 1993 na Nkata 1993). Utafiti huu ulikusanya data kwa kutumia mbinu mbili. Kwanza, tulianza na mbinu ya maktabani, ambapo tuliweza kusoma, kutathmini na kuhakiki vitabu vinne vya kiada vya Kiswahili vya shule za msingi. Baadaye ulifanyika utafiti wa uwandani, ambapo watafitiwa walijaza hojaji na wengine tulihojiana nao. Vifaa vya utafiti vilivyotumika ni shajara, kalamu, karatasi, daftari, simu ya mkononi, hojaji, dodoso, kompyuta na vifaa vyake. Eneo la utafiti lilikuwa ni mkoa wa Dar es Salaam. Kuteuliwa kwa eneo hili kulitokana na kuwapo kwa makampuni mengi ya uchapishaji, asasi na vyombo vya kielimu katika jiji hilo. Nadharia ya “mawazo ni ya mwandishi, kitabu ni cha mhariri” ilitumika hadi kufanikisha utafiti huu. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mkabala wa kitaamuli ambapo data zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo, majedwali na vielelezo. Baada ya hatua zote kukamilika, tuligundua kuwapo kwa makosa mengi ya kiuhariri katika vitabu vya kiada vya Kiswahili nchini Tanzania. Kwa mfano, makosa ya matumizi ya herufi kubwa, vifupisho na finyazo, upangiliaji wa vichwa vya habari na makosa ya istilahi. Makosa hayo yanaonekana kusababishwa na mambo ya kiufundi na ya kiutawala. Mwisho tumependekeza mbinu za utatuzi wa makosa hayo. Mwishoni tunapendekeza maeneo yanayohitaji utafiti zaidi.
Description
Kinapatikana Maktaba ya Dkt Wilbert Chagula, Kitengo cha East Africana, Classmark (THS EAF PN162.J67)
Keywords
vitabu, matatizo, uhariri, kiada
Citation
Joster, F. (2015) Matatizo ya kiuhariri katika vitabu vya kiada vya Kiswahili nchini Tanzania. Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.