Mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena.

dc.contributor.authorSehelele, Magdalena
dc.date.accessioned2020-02-19T06:59:09Z
dc.date.available2020-02-19T06:59:09Z
dc.date.issued2011
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025M43)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena. Ingawa kuna tafiti zilizofanywa na Nurse (1979) na Priebusch (1935) kuhusu mfumo wa njeo na hali katika lugha hii, bado tafiti hizi zilikuwa za kiwango cha arabi na hivyo hazikufafanua kwa kina mfumo wa njeo na hali wa lugha ya Ki-bena. Utafiti huu ulilenga kuchunguza mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena hasa lahaja ya Ki-Lupembe kwa kuangalia ni vipengele vipi vya kimofolojia hubainisha njeo na hali. Pia, utafiti ulilenga kuchunguza mchango wa vielezi vya wakati na hali katika kubainisha muda na hali mahususi ya tukio katika sentensi yakinishi za Ki-bena. lli kutimiza malengo ya utafiti huu nadharia ya Ulalo iliyoasisiwa na Reichenbach (1947) ndiyo iliyotumika kuchambua data za ulafiti nadharia hii imefaa kutumiwa katika kuelezea mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena baada ya kufanyiwa marekebisho na wataalamu kama, Johnson (1977), Smith (1978) na Besha (1985). Data zilizotumiwa katika utafiti huu zilikusanywa kutoka katika vijiji vitatu vilivyopo katika tarafa ya Lupembe wilayani Njombe. Vijiji hivyo ni Kanikelele, Soliwaya na Lupembe Data za utafiti zilikusanywa kwa njia ya, mahojiano, dodoso na uchambuzi matini. Utafiti huu umebainisha kuwa katika lugha ya Ki-bena kuna mofimu sita (6) za njeo ambaza hujitokeza kabla ya mzizi wa kitenzi.Vile vile kuna mofimu nne (4) za hali ambapo mofimu tatu (3) hujitokeza baada ya mzizi wa kitenzi na mofimu moja (1) ambayo ni ya hali endelevu hujitokeza kabla ya mzizi wa kitenzi Utafiti huu pia umebainisha kuwa mofimu za njeo na hali hutumiwa pamoja na vielezi vya wakati na hali ili kubainisha muda na hali mahususi ya tukio.en_US
dc.identifier.citationSehelele, M. (2011). Mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena. Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/7218
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectBena languageen_US
dc.subjectBantu languageen_US
dc.titleMfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena.en_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Sehelele 2011.pdf
Size:
82.62 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: