Dhima za wahusika wa kingano katika ushairi andishi wa Kiswahili uchunguzi wa diwani za Chungu Tamu (1985) na Dhifa (2008)
Loading...
Date
2017
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza Dhima za Wahusika wa Kingano katika Ushairi Andishi wa Kiswahili. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka katika diwani za Chungu Tamu (Mvungi, 1985) na Dhifa (Kezilahabi, 2008). Uchambuzi wa data za utafiti huu uliongozwa na misingi ya nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva. Nadharia hii imesaidia kujadili malengo ya utafiti ambayo ni kubainisha aina za wahusika wa kingano katika diwani teule, kujadili sifa za wahusika wa kingano wanaopatikana katika diwani teule na kuchunguza dhima za wahusika wa kingano wanaopatikana katika diwani teule.
Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa diwani za Chungu Tamu na Dhifa zimesheheni matumizi ya wahusika wa kingano wa aina mbalimbali ambao ni pamoja na wanyama, ndege wadudu na wahusika dhahania. Pia matokeo yanaonesha sifa hasi na chanya ambapo kutokana na sifa walizopambanuliwa nazo wahusika hawa; wanajamii wanajifunza mambo mbalimbali.
Baadhi ya mambo hayo ni: kuwa na upendo wa kweli kwa wanajamii wenzao, kuwa wavumilivu, kuwa na umoja wao kwa wao, kuwaepuka viongozi wanaoongoza kwa mabavu, kuwaepuka wanajamii wasio waaminifu katika ahadi zao pamoja na kuangalia yale yanayofaa kufanya mbele za watu ili kulinda maadili ya jamii. Vilevile matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa matumizi ya wahusika wa kingano yana dhima mbalimbali ambazo ni: kuwafanya wasomaji kuwa watu wenye kufikiri ili kuelewa alichokusudia mtunzi, kuwajengea wanajamii ujasiri wa kufanya mambo makubwa hata yale yanayoonekana kutowezekana, kuwafundisha wanajamii faida za kuwa na umoja, ushirikiano na uhusiano kati yao, kuwajengea watunzi uhuru kwa kutomkwanza yeyote katika jamii kutokana na uandishi wao.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.N548)
Keywords
Swahili poetry, Character and characteristics in literature, Diwani ya chungu Tamu (1985), Diwani ya Dhifa (2008)
Citation
Nikundiwe, R. (2017) Dhima za wahusika wa kingano katika ushairi andishi wa Kiswahili uchunguzi wa diwani za Chungu Tamu (1985) na Dhifa (2008). Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.