Factors influencing the utilization of antenatal care services in Tabora region: a case of Tabora Municipality, Tanzania
Loading...
Date
2018
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulichunguza vipengele vinavyoathiri utoaji wa huduma zinazowalenga wanawake wajawazito kabla yakujifungua katika Manispaa ya Tabora.Utafiti huu ulikuwa na malengo manne ambayo ni: kiwango cha uelewa wa wanawake kuhusu huduma zinazolenga wajawazito kabla ya kujifungua katika Manispaa ya Tabora, uwepo wa wahudumu wa afya na vifaa tiba kwa ajili ya utoaji wa huduma kwa wajawazito katika Manispaa ya Tabora. Vitu vinavyoathiri utoaji wa huduma kwa wajawazito katika Manispaa ya Tabora na mikakati iliyopo kwa ajili yakuboresha huduma kwa wajawazito katika Manispaa ya Tabora.Utafiti huu ulitumia mkabala wa ki idadi na kimaelezo katika kuchanguza tatizo la utafiti.Sampuli ya watafiti wa iliyotumika katika utafiti huu ilikuwa na watafiti waambao ni wanawake wanaopata huduma ya afya ujauzito katika vituo vya afya, wanawake wasiopata huduma ya afya ya ujauzito katika vituo vya afya, wahudumu wa afya, wakuu wa vitengo vya huduma ya afya na wakunga wa jadi. Utafiti huu ulitumia usampulishaji tabakishi kuteua watafiti wa wapatao 455.Mbinu zilizotumika kukusanya data nihojaji, mahojiano na ushuhudiaji.Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa taarifa mbalimbali zakijamii zawatafiti wakuhusu umri, elimu, hali ya ndoa, kipato, makazi na dini pamoja na usawa vinaashiria mambo yanayo athiri utoaji wa huduma kwa waja wazito katikaManispaa ya Tabora.Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa jamii ipewe maarifa kuhusu huduma zinazo walenga waja wazito, waja wazito waelezwe faida za kupata huduma ya afya kipindi cha ujauzito pamoja na muda muafaka wa kuanza kuhudhuria kiliniki kwa mjamzito ilikupata huduma za afya. Hata hivyo, miundo mbinu hafifu ya afya, wahudumu wachache, upungufu wa dawa na vifaa tiba, usimamizi mbovu wa afya katika ngazi zote na mgawanyo usiofaa wa rasilimali tiba unaathiri utoaji wa huduma kwa wajawazito kwa kiwango kikubwa. Utafiti huu unapendekeza mambo ya muhimu ya kuzingatia katika kuboresha huduma ya afya kwa wajawazito. Pia inapendekezwa kuwa kuwepo na ushirikikiano wa utoaji huduma kati ya huduma kwa waja wazito na huduma nyingine za afya kama vile utoaji wa huduma yakinga ya magonjwa kwa watoto na uzazi wa mpango.Elimu hii inapaswa kuenezwa kwa walengwa wote wanaohitaji huduma ya waja wazito badala yakutolew akwa wale tu wanaohudhuria kiliniki. Akina mama waja wazito wanapaswa kuelimishwa na kupewa ushauri nasaha kuhusu umuhimu wa kuhudhuria kiliniki kipindi chote cha ujauzito hasa kila wanapo kwenda kuhudhuria kiliniki. Mikutano mbalimbali inayohusu huduma za afya kwa mama mjamzito zitolewe kwa viongozi mbalimbali wa kijamii ilikusaidia kusisitiza umuhimu wa utoaji huduma za afya kwa wajawazito. Pia inapendekezwa kuwa watoa huduma ya afya kwa wajawazito waboreshewe mazingira yakufanyia kazi kama kuwasomesha zaidi na kuwasimamia iliwaweze kutoa huduma nzuri na sahihi kwa watejawao.Serikali iendeleze mikakati yake yakuboresha uwepo na urahisi wa kupatikana kwa huduma ya afya kwa wajawazito. Pia wakunga wa jadi wanapaswa kubainishwa na kuelekezwa mahali pa kuwapeleka wajawazito inapotokea wakapata uchungu wa muda mrefu au dharura nyingine. Mwisho, serikali ihakikishe kuna sera kuhusu huduma ya afya kwa mama mjamzito.
Description
Available in printed form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF RG940.T34K394)
Keywords
Maternal health services, Prenatal care, Tabora municipality, Tanzania
Citation
Kawiche, L (2018) Factors influencing the utilization of antenatal care services in Tabora region: a case of Tabora Municipality, Tanzania.Doctoral dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.