Matumizi ya lughatandawazi katika simu za kiganjani: changamoto katika lugha ya Kiswahili

No Thumbnail Available
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Mfumo wa lugha umechukua sura tofauti katika zama hizi za sayansi na teknolojia hasa katika mitandao ya mawasiliano. Kutokana na kupanuka kwa utandawazi, mtindo mpya wa matumizi ya lugha katika simu za kiganjani umezuka na kuleta changamoto katika Isimujamii, mawasiliano na katika Kiswahili kwa ujumla. Mabadiliko ya sarufi ni moja ya changamoto hizo. Ili kujua chanzo na athari za mabadiliko hayo, utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza matumizi ya Lughatandawazi na athari zake katika Kiswahili katika kuandika ujumbe wa simu za kiganjani. Utafiti umeongozwa na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano (NKM), yenye lengo la kueleza sababu za kubadili mtindo wa matamshi wakati wa mawasiliano ya kijamii na kuangalia athari zake katika jamii. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, katika wilaya ya Mjini. Jumla ya watafitiwa 98 walishiriki katika utafiti huu, ambao wametoka katika shule za Sekondari za Kiembesamaki, Lumumba na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, mahojiano na uchunguzi. Matokeo yameonesha kuwa Lughatandawazi inaharibu sarufi na tahajia ya Kiswahili. Pia, imebainika kuwa chanzo kikuu cha kutumia mtindo huo ni kupunguza gharama za kutuma ujumbe. Kutokana na matokeo hayo, inapendekezwa kuwa vianzishwe vitengo maalumu vitakavyoshughulikia mitindo mbalimbali inayoibuka katika lugha kwa lengo la kuihifadhi na kuidhibiti mitindo lugha.
Description
Keywords
Swahili language, Grammar, Text messages (cell phone systems), Instant messaging
Citation
Mohammed, N. A (2013) Matumizi ya lughatandawazi katika simu za kiganjani: changamoto katika lugha ya Kiswahili, Tasinifu ya M.A. (Kiswahili), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)