Matumizi ya kiswahili na athari zake katika lugha ya Kirombo wilayani Rombo.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umefanywa juu ya matumizi ya lugha ya Kiswahili na athari zake katika lugha ya Kirombo Wilayani Rombo. Athari zilizotafitiwa ni zile za msamiati pamoja na kuangalia sababu za matumizi ya lugha hizo katika eneo husika. Data na taarifa za utaflti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, hojaji na ushuhudiaji. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba lugha ya Kirombo inatumika katika maeneo rasmi kama vile kazini na maeneo yasiyo rasmi kama vile katika mikutano ya koo. Matokeo yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili inatumika katika maeneo ya nyumbani, sokoni, na katika michezo kwa upande athari ya Kiswahili, katika Kirombo utafiti umebaini kuwa baadhi ya msamiti kutoka lugha ya Kiswahili umekopwa na kutumika katika lugha ya Kirombo. Mbinu zinazotumika katika kukopa msamiati wa Kiswahili ni pamoja na kuchukuliwa bala kufanyiwa marekebisho, kuongezewa viambishi, na kudondoshwa kwa viambishi. Sababu mbalimbali za matumizi ya lugha ya Kiswahili au lugha ya Kirombo katika maeneo mbalimbali ya mawasilianao. Sababu za kutumia lugha ya Kirombo, ni lugha inayowatambulisha kuwa Wachaga wa Rambo, ni lugha inayowaweka pamoja, na inatunza utamaduni wao. Wakati Kiswahili kinatumiwa kwa sababu yapo maeneo arnbayo huwezi kuzungumza Kirombo mfano katika biashara. Uwepo wa misamiati michache ya Kirombo hufanya lugha ya Kiswahili kitumike. Mwisho maeneo yaliyopendekezwa kwa ulafiti zaidi ni pamoja athari za Kirombo kwenye lugha ya Kiswahili, na athari za Kiswahili kwenye kirombo katika matamshi.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8701.A66)
Keywords
Swahili language, Rombo language, Rombo district
Citation
Apolinari, M. (2011). Matumizi ya kiswahili na athari zake katika lugha ya Kirombo wilayani Rombo. Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.