Siasa katika ushairi wa kezilahabi :Uchunguzi wa Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008)

No Thumbnail Available
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kubainisha masuala ya kisiasa yanayojitokeza katika ushairi wa Kezilahabi. Lengo hili limeweza kufanikiwa kutokana na kukamilika kwa malengo mahususi yaliyohusu kubainisha dhamira mbalimbali za kisiasa zinazojitokeza katika diwani teule, kubainisha mbinu za kifasihi zinazotumika kueleza masuala ya kisiasa katika diwani teule na kutathimini mtazamo wa mwandishi katika maendeleo ya masuala ya kisiasa kama yanavyojitokeza katika diwani hizo. Maandiko na machapisho mbalimbali juu ya ushairi wa Kezilahabi yamepitiwa chini ya uongozi wa nadharia ya Simiotiki. Utafiti umetumia mbinu ya uchambuzi matini katika kukusanya data za msingi za utafiti huu pamoja na data fuatizi kutoka maandiko mbalimbali. Uchambuzi wa data umeongozwa na mbinu ya uchambuzi wa kifasihi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, Kezilahabi anazungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa katika diwani teule, tofauti na maelezo ya Frolova (2003) kwamba, Kezilahabi hazungumzii siasa katika Karibu Ndani (1988). Katika diwani hii mshairi ameibua masuala mbalimbali ya kisiasa yatokanayo na siasa za Azimio la Arusha (1967). Miongoni mwa masuala hayo ni ujenzi wa jamii mpya kama dhamira kuu huku ikijengwa na dhamira ndogondogo kama vile uongozi, utekelezaji wa maamuzi; maamuzi ya kuanzisha Azimio la Arusha, utekelezaji wa Azimio la Arusha, ugumu wa maisha wakati wa Azimio la Arusha na kupambana dhidi ya ukoloni mamboleo. Vilevile katika diwani ya Dhifa (2008), mshairi anaongelea juu ya siasa za kidemokrasia, ubinafsishaji na uwekezaji, elimu na ualimu, jinsia, siasa za vyama vya kisiasa, matatizo ya watumishi wastaafu, uongozi katika jamii, uongozi na ujana, uongozi ni mtaji pamoja na masuala ya rushwa na ufisadi. Matokeo ya utafiti pia yamebaini kwamba, kwa kiasi kikubwa msanii anatumia mbinu za kisanaa za fasihi simulizi katika kufikisha ujumbe kwa hadhira lengwa. Mbinu hizo ni usimulizi, ucheshi, taswira na ishara, wahusika, tanakali-sauti na ukimya. Mbinu hizi ni muhimu katika kuibua dhamira zihusuzo masuala ya kisiasa katika ushairi wa Kezilahabi. Matokeo ya utafiti yanabainisha kwamba, uelewekaji wa ushairi wa Kezilahabi utategemea umahiri wa wasomaji wake katika kufumbua taswira na ishara mbalimbali zinazojengwa kapitia mbinu mbalimbali za kifasihi simulizi.Mwisho limetolewa hitimisho kuu la utafiti, lililoainisha nyanja mbalimbali za kiutafiti zinazoweza kuibuliwa katika ushairi wa Kezilahabi na ule wa kisasa/majaribio kwa ujumla.
Description
Available in print form
Keywords
Swahili poetry, Karibu ndani (1988),, Dhifa (2008), Kezilahabi
Citation
Omary, M(2011)Siasa katika ushairi wa kezilahabi :Uchunguzi wa Karibu Ndani (1988) na Dhifa (2008), master dissertation, University of Dar es Salaam (available athttp://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx?parentpriref=)