Tathimini ya athari ya mgogoro wa ushairi wa Kiswahili watunzi wa sasa nchini Tanzania: mifano kutoka shindano la ushairi la tunzo ya Ebrahim Hussein,2015 na 2016
Loading...
Date
2018
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza mgogoro wa Kiswahili nchini Tanzania. Utafiti umejikita katika kutathimini athari za mgogoro huo watunzi wa sasa kupitia watunzi washindano la Ushairi la Tunzo ya Ebrahim Hussein kwa mwaka 2015 na 2016.Utafiti huu uliongozwa na malengo mahusussi matatu ambayo ya Kubainisha mrengo wa utunzi uliojitokeza zaidi katika shindano la Ushairi la Tunzo ya Ebrahim Hussein kwa mwaka 2015 na 2016, kueleza sababu zilizowafanya watunzi wa mashairi ya shindano la Ushairi la Tunzo ya Ebrahim Hussein kwa mwaka 2015 na 2016 kutunga tungo zao kwa mirengo tofauti, na kujadili dhamira za tungo zilizotungwa kwa mirengo katika shindano la Tunzo la Ebrahim Hussein Ebrahim Hussein kwa mwaka 2015 na 2016.Data za Utafiti huu zilikusanywa maktabani na Uwandani.Maktabani ,zilipatikana kutoka kaitka Diwani mbili za Tunzo ya Mashairi ya Ebrahim Hussein 2015 na 2016.Pia kwa kusoma maandiko mbalimbali yanayohusiana na Ushairi wa Kiswahili.Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu za uchambuzi wa mashairi pamoja na majadiliano na usaili.Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kujiegemeza katika nadharia mbili za Jadi ya Ushairi wa Kiswahili iliyoasisiwa na William Hichens (1941). Nadharia ya pili iliyoongoza utafiti huu ni sosholojia ya Fasihi iliyoasisiwa na Bronislaw Malinowski (1922). Uwasilishaji wadata ulifanywa kwa makabala wa kitaamuli pamoja na mkabala wa kiidadi.Matokeo ya Utafiti huu yameoneshwa kuwa watunzi 57 kati ya 67 walitunga mashairi yao kwa ,mrengo wa kimapokeo na watunzi 10 waliandika mashairi yao kwa mrengo kwa kisasa.katika utafiti huu pia imebainika kuwa watunzi wa m,ashairi yao kwa mrengo wa kisasa wapo waliochanganya utunzi wao kwa kujuimuisha mbinu za kimapokeo.Aidha, Utafiti huu pia umeabinika kuwapo kwa sababu tofauti kwa watunzi wa mirengo hii miwili katik utunzi wao.Baadhi ya sababu za watunzi wa mrengo wa kisasa nikutaka kuyatambulisha zaidi maisha ya kisasa,kuonesha umahiri wa kutunga kwa mirengo miwili tofauti na kutaka kufanya mapinduzi kaitka ushairi wa Kiswahili.sababu za watunzi wa mashairi wa mrengo wa kimapokeo ni pamoja na kutaka Kuenzi Ushairi halisi wa Kiswahili,Kuandika tungo zenye mvuto na ukubalifu na kuatafuta ushindi katika shindano lililotafitiwa.Dhima hizo zimetwanyika kaitka sekta za kijamii,kiuchumi,kisasa ,kiteknolojia na kiutamaduni. Hitimisho, Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa bado upo mgogoro kwa watunzi wa sasa wa mashairi ya Kiswahili nchini Tanzania.Hata hivyo,mgogoro huo sio mpevu sana kama ulivyokuwa mnamo 1970 na 1980. Athari za mgogogro huu bado zinajidhililisha kaitka tungo na kauli za watunzi wa sasa wa mshairi nchini Tanzania na kusababisha tungo zao kufumbata taathira za mgogoro uliyotamalaki miaka iliyotajwa hapo juu. Inapendekezwa kuwa watafiti wengine wachunguze mgogoro wa Ushairi wa Kiswahili ili kubaini iwapo umeudumaza au kuuendeleza ushairi huo.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL1126.T34A838)
Keywords
Swahili poety, Poety Modern, Poety, Tanzania
Citation
Abdallah,A (2018) Tathimini ya athari ya mgogoro wa ushairi wa kiswahili watunzi wa sasa nchini Tanzania: mifano kutoka shindano la ushairi la tunzo ya Ebrahim Hussein,2015 na 2016,Tasnifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.