Mwingiliano wa matumizi ya lugha bain a ya kiswahili na kimeru na athari zake katika Lugha hizo
dc.contributor.author | Luka, Eva | |
dc.date.accessioned | 2020-04-30T20:54:24Z | |
dc.date.available | 2020-04-30T20:54:24Z | |
dc.date.issued | 2012 | |
dc.description | Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, | en_US |
dc.description.abstract | Utafiti huu unahusu Mwingiliano wa Matumizi ya Lugha baina ya Kiswahili na Kimeru na Athari zake katika Lugha hizo. Utafiti huu umejikita katika malengo makuu mawili ambayo ni kubainisha na kufafanua maeneo ya matumizi ya lugha ya Kiswahili na lugha ya Kimeru na kubainisha na kueleza athari za mwingiliano baina ya lugha hizo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uchanganuzi wa kimaeneo ambayo iliasisiwa na kutumiwa na Fishman 1972. Nadharia hii inaelezea mazoea ya wazungumzaji ya kupenda kuchagua kutumia lugha fulani katika eneo fulani na lugha nyingine itumike katika eneo jingine. Utafiti huu umefanyika katika vijiji vya Nndatu, Poli, na Nkoaranga ambavyo viko katika kata ya Poli wilaya ya Arumeru, mkoa wa Arusha. Watafitiwa 60 walihusika katika utafiti huu ambapo usampulishaji nasibu tabakishi ulitumika kwa kuzingatia vigezo vya umri na jinsi. Katika ukusanyaji wa data, mbinu za hojaji, mahojiano na ushuhudiaji zilitumika. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba katika maeneo ya matumizi yaliyofanyiwa utafiti ya mtaani, sokoni, kazini na maeneo ya burudani, imedhihirika kwamba lugha ya Kimeru inatumiwa na wazungumzaji wengi katika maeneo yote ya matumizi. Matumizi haya ya Kimeru yanaeleza kwamba Kimeru bado kinadumishwa katika maeneo hayo. Lugha ya Kiswahili inatumiwa na wazungumzaji wachache wa Kimeru. Hata hivyo mwingiliano huu wa Kiswahili na Kimeru umesababisha kuwepo kwa athari za kifonolojia na kimsamiati. Athari za kifonolojia zinasababishwa na tofauti ya idadi ya konsonanti baina ya Kiswahili na Kimeru. Athari za kimsamiati zinatokana na kukosekana kwa maneno ya Kimeru ya kuelezea dhana ngeni za Kiswahili, hivyo kufanya lugha ya Kimeru kukopa maneno mengi kutoka Kiswahili | en_US |
dc.identifier.citation | Luka, E (2012) , Mwingiliano wa matumizi ya lugha bain a ya kiswahili na kimeru na athari zake katika Lugha hizo,Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam | en_US |
dc.identifier.uri | http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/10602 | |
dc.language.iso | sw | en_US |
dc.publisher | University of Dar es Salaam, | en_US |
dc.subject | Swahili language | en_US |
dc.subject | Swahili | en_US |
dc.subject | kimera | en_US |
dc.title | Mwingiliano wa matumizi ya lugha bain a ya kiswahili na kimeru na athari zake katika Lugha hizo | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |