Matumizi ya lugha ya kiswahili isiyo sanifu katika vyombo vya habari nchini Tanzania mifano kutoka katika redio
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia “Matumizi yasiyo sanifu ya lugha ya Kiswahili katika Vyombo vya Habari Nchini Tanzania: Mifano kutoka katika Redio”. Aidha, vituo vya Redio vilivyoshughulikiwa ni East Africa Redio, Clouds FM na Radio One Stereo. Utafiti huu umefanyika Dar es Salaam katika wilaya ya Kinondoni na Ilala na Tanga katika wilaya ya Tanga mjini. Malengo ya utafiti huu ni kuainisha matamshi na msamiati wa lugha ya Kiswahili usio sanifu unaotumiwa wa watangazaji wa redio nchini Tanzania. Pia ulilenga kupendekeza mbinu za kupunguza tatizo la upotoshaji wa matumizi sanifu ya lugha ya Kiswahili ili kukuza lugha ya Kiswahili sanifu. Ili kufikia malengo hayo, utafiti huu umetumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa data zikiwemo; hojaji, mahojiano na usikilizaji. Nadharia zilizotumika katika utafiti huu ni Nadharia Kidhi Mawasiliano na Nadharia ya Usukuku. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha msamiati na matamshi yasiyo sanifu yanayotumiwa na watangazaji wa redio nchini Tanzania. Aidha msamiati huo usio sanifu ni msimbo, Kiingereza, Kiarabu na maneno ya mtaani. Pia, matamshi potofu katika maneno ya Kiswahili ni ukiukwaji wa udondoshaji, uchopekaji, ubadilishaji sauti (fonimu) na uyeyushaji wa maneno sanifu ya Kiswahili. Aidha, utafiti huu umependekeza mbinu za kupunguza tatizo la upotoshaji wa watu.