Je, Kinyakyusa kina mkazo au toni?
No Thumbnail Available
Date
2013
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Wataalamu wengi wa fonolojia, wanaelekea kukubaliana kwamba Lugha za ki-Bantu ziko katika makundi manne: lugha zenye toni asilia, lugha zenye viinitoni, lugha zilizo kati ya kuwa na viinitoni na kuwa na mkazo na lugha zenye mkazo peke yake. (taz. McCawley 1974 na Massamba 2011:176-177). Hata hivyo, ni lugha chache zilizochunguzwa vipambasauti vyake vya toni na mkazo, na kubainika kuwa kuna lugha zenye toni asilia, viinitoni na mkazo peke yake, lakini lugha zenye viinitoni na mkazo hakuna iliyobainika katika kundi hilo. Hivyo, utafiti huu unahusu mkazo na toni katika kiwango cha neno na tungo katika Kinyakyusa ili kuziba pengo hili. Data zilizotumika ni nomino, vivumishi, vitenzi, viwakilishi na vielezi, pamoja na tungo virai na sentensi zilizokusanywa katika kijiji cha Ibula, Kasyeto na Lwifwa tarafa ya Ukukwe, Msasani na Pakati Wilayani Rugwe, Mkoani Mbeya. Data zilikusanywa kwa njia za mahojiano, ushiriki na ushuhudiaji kisha kurekodiwa kwa kinasasauti. Katika uchanganuzi wa data tumetumia nadharia ya FM iliyoasisiwa na Liberman & Prince (1977) na FVH iliyoasisiwa na Goldsmith (1976) ambapo vipengele vya kifonolojia vimewakilishwa katika rusu huru. Utafiti huu umegusia vipengelele vya vya irabu, konsonanti, silabi na mambo yanayodhibiti ruwaza za mkazo na toni. Aidha, imebainika kuwa Kinyakyusa kina mkazo huru, unaoangukia silabi yoyote katika neno na katika kiwango cha tungo, kikonyo dada cha pili kina nguvu kuliko cha kwanza katika kategoria ya kirai na kileksika. Vilevile, imebainika kuwa Kinyakyusa kina maegemeomkazo huru na funge. Kwa upande mwingine imebainika kuwa Kinyakyusa kina toni zinazochombezwa na kiinitoni. Kiinitoni chake kinahusishwa na tonijuu. KTM cha nomino za lugha hii ni JC, CJC na CJ, na CJC kwa upande wa vitenzi. Aidha, kuna kanuni zimejibainisha, nazo ni: upachikaji kiinitoni, udondoshaji wa kiinitoni, mbiruko nyuma wa kiinitoni na usambaaji tonijuu kulia na kanuni za uhusishaji KTM na kiinitoni. Matokeo ya utafiti huu yanakanusha madai yanayosema: lugha ya Kinyakyusa ina mkazo peke yake na haina toni, bali unaonesha kuwa lugha ya Kinyakyusa ina mkazo na toni na hivyo kuingia katika kundi la tatu la lugha za Kibantu lenye lugha ambazo ziko kati ya kuwa na viinitoni na kuwa na mkazo.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark
(THS EAF PL8549M37)
Keywords
Nyakyusa language
Citation
Masuba, S. (2013) Je, Kinyakyusa kina mkazo au toni?, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.