Toni katika vitenzi vya kimochi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasnifu hii imelenga kuelezea utafiti uliochunguza “Toni katika Vitenzi vya Kimochi” kwa kutumia kiunzi cha nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru katika uchanganuzi wa data. Nadharia hii iliasisiwa na Goldsmith (1976) ambapo vipengele vya kifonolojia vimewakilishwa katika rusu huru. Utafiti huu umegusia vipengele vya kifonolojia kama vile irabu, konsonanti, silabi na michakato ya kifonolojia inayoathiri ruwaza za toni. Data zilizotumika katika utafiti huu ni vitenzi visoukomo vilivyokusanywa uwandani katika vijiji vya Tsuduny, Shia, Kidia, Mowo na Mbokomu vilivyoko katika Kata ya Old-Moshi Mashariki, Wilayani Moshi vijini, Mkoa wa Kilimanjaro. Data zilikusanywa kwa hojaji, mahojiano na kurekodiwa kwa kinasasauti aina ya MP3 IC recorder na kuchambuliwa kwa mbinu ya uchanganuzi wa data kimada. Imebainika kuwa toni za lugha hii ni tabirifu ambapo kitenzi huanza na tonichini katikati tonijuu na mwisho tonichini. KTM ni CJC. Utokeaji wa toni katika vitenzi visoukomo vya lugha hii hutegemea idadi ya silabi za shina la kitenzi. Kiinitoni katika vitenzi visoukomo huangukia katika silabi ya mwisho kasoro moja. Na kiinitoni hicho kinahusishwa na tonijuu ya KTM.
Description
Available in print form, University of Dar es Salaam at Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8516.974N44)
Keywords
Mochi language, Chapa language
Citation
Nelson, C(2013)Toni katika vitenzi vya kimochi, Master dissertation, University of Dr es Salaam, Dar es Salaam