Tamthilia ya kiswahili na mabadiliko ya dhamira

Loading...
Thumbnail Image
Date
1979
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Thanifu hii itojadili mabadiliko ya dhamira katika tamthilia za Kiswahili kati ya 1957 na 1975 kwa kutumia mtindo wa uchambuzi wa nadharia ya kihadhira. Mazigowanya dhamira za tamthiria hizo katika mafungu mawili. La kwanza ni zile tamthilia zilizoandikwa katika kipindi cha kabla ya uhuru (1957 hadi 1961) na la pili ni lile la tamthilia zilizoandikwa katika kipindi cha uhuru na baada ya uhuru. Tasnifu hii itajadili kuwa dhamira za tamthilia za kipindi cha kabla ya uhuru hazikushughulikia migogoro halisi ya jamii ya wakati ule, ana kwamba baadhi ya tamthilia za kipindi hicho zilijaribu kuonyesha mabadiliko ya uchumi kutoka ule wa asili hadi wa ukoloni, lakini tamthilia hizi hazionyeshi wazi wazi athari za ubepari. Aidha itajadili kwamba dhamira za tamthilia za kipindi cha uhuru na baada ya uhuru zilijadili matatizo mhimu ya baada ya uhuru na kuwa zinaonyesha wazi wazi mfumo na uchumi wa ujamaa. Sura ya kwanza itajadili mijadala ya tasinifu na stindo wa uchambuzi wa nadharia ya kidhamira ambao ndio utakaotumiwa katika tasnifu hii. Sura ya pili itahusu uhakiki uliokwisha fanywa na wahakiki wengine kuhusiana na tanmthilia zitakazochambuliwa katika tasnifu hii. Itaonyesha kuwa wengi wa wahakiki tahakiki zao zimekuwa za tamthilia moja moja na za jumla; hazikuwa na lengo la kujadili dhamira peke yake. Aidha itaonyesha kuwa hatak wahakiki waliojadili Zaidi ya tamthiia moja uchambuzi wao haukuhusu kipengele cha dhamira peke yake, na kwamba uchambuzi wao waliofanya kuhusu dhamira haukuonyesha mabadiliko ya dhamira katika nyakati mbali mbali. Sura ya tatu itajadili dhamira za tamthilia za kipindi cha kabla ya uhuru. Itajadili kuwa dhamira za kipindi hiki hazikuhusisha matatizo mhimu na makubwa ya wakati huo; na kwamba zile zilizojaribu kuonyesha athari za ukoloni mkonge na mfumo wa kibepari majaribio haya hayakufanikiwa kwa sababu ya kutumia mtindo wa vichekesho, madhuminui ya tamthilia za maandishi katika kuandika tamthilia hizo. Sura ya nne itachambua tamthilia za kipindi cha uhuru na baada ya uhuru, itajadili ya kwamba tamthilia za wakati huo zilihusisha matatizo halisi ya jami ya wakati huo. Itahusu dhamira za utamaduni na ukombozi. Itaonyesha kwamba tamthilia zenye dhamira ya utamaduni zitaonyesha athari ya ukombozi na kumulika madhara ya mfumo wa kibepari. Kuhusu dhamira ya ukombozi surah ii itaonyesha umuhimu uliowekwa katika itikadi, moja, silaha na mbinu za kivita. Sura ya tano itajadili dhamira ya ujenzi wa jamii mpya. Itaonyesha kwamba kimsingi mgogoro uliopo ni ule wa misingi ya ubepari dhidi ya ujamaa na kuonyesha jitihada inayofanywa na waandishi wa tamthilia katika ujenzi wa jamii mpya na matatizo yanayotokana na jitihada zao. Sura ya sita itakuwa ni hitimisho la tasnifu. Itatoa muhutaasari wa yote yaliyojadiliwa na kuonyesha mwelekeo ambao tamthilia za Kiswahili zimeelekea katika jamii.
Description
Inapatikana Maktaba ya Dkt Wilbert Chagula, Kitengo cha East Africana, Classmark ( THS EAF PN2990.T3K5)
Keywords
Swahili drama, History and criticism
Citation
Kiango, S. D (1979) Tamthilia ya kiswahili na mabadiliko ya dhamira, Tasinifu ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam