Riwaya mpya ya kiswahili na masuluhisho ya changamoto za utandawazi

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza riwaya mpya ya Kiswahili na masuluhisho ya changamoto za utandawazi riwaya teule zikiwa Babu Alipofufuka (2001) na Bina-Adamu! (2002). Utafiti huu umechunguza changamoto mbalimbali za utandawazi, masuluhisho yanayotolewa na waandishi kuhusiana na changamoto za utandawazi na mitazamo ya waandishi katika kukabiliana na changamoto hizo. Ili kufikia lengo hilo, mbinu kuu ya ukusanyaji wa data iliyotumika ni usomaji wa matini. Pamoja na mbinu hiyo, vifaa mbalimbali kama vile kalamu na shajara, kinyonyi na kompyuta vilitumika. Aidha, uchambuzi na ufasili wa data ulielemea katika nadharia ya uhalisia. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa waandishi Mohamed (2001) na Wamitila (2002) wamejadili na kutoa masuluhisho mbalimbali kuhusiana na changamoto za utandawazi. Masuluhisho hayo yapo katika madaraja ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kiteknolojia, kimazingira na ya kijamii kwa ujumla. Lakini tunaweza kusema kwa ujumla wake kuwa masuluhisho haya yamekitwa katika mitazamo ya ndani ya Afrika. Waandishi wanapendekeza kuwa ili Afrika ijinasue kutokana na matatizo mbalimbali yaliyosababishwa na utandawazi basi haina budi kujipanga upya na kuelekeza juhudi zake za pamoja katika kuhakikisha Afrika inajitegemea kwa kila jambo. Aidha suala la msingi linalosisitizwa na waandishi ni kuona Afrika ikichanua yenyewe bila masharti na maelekezo kutoka nchi za Magharibi kupitia vyombo vyao vinavyomiliki mwenendo wa siasa, fedha na uchumi wa kiulimwengu. Mwisho utafiti huu unapendekeza kufanyika tafiti zaidi kuhusiana na mchango wa fasihi andishi ya Kiswahili katika kukabailiana na matatizo ya utandawazi. Aidha, suala la mafungamano baina ya Afrika na nchi zilizoendelea kiuchumi lifanyiwe mjadala wa kutosha. Mwisho viongozi wa kisiasa wa Afrika waamke kutoka usingizini na kusimama imara kutoka na tishio la utandawazi.
Description
Keywords
Swahili literature, Globalization
Citation
Libui, O. S (2012) Riwaya mpya ya kiswahili na masuluhisho ya changamoto za utandawazi, Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx)