Uzingativu wa kanuni ya uhusiano katika mahubiri ya dini ya kikristo

Loading...
Thumbnail Image
Date
2017
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Tasinifu hii imejadili ‘Uzingativu wa Kanuni ya Uhusiano Katika Mahubiri ya Dini ya Kikristo’. Hivyo, mahubiri manne tofauti yamechunguzwa. Aidha, kutokana na malengo ya utafiti huu, tasinifu imejadili namna mahubiri hayo yanavyoizingatia kanuni ya uhusiano kwa kuviangalia vipengele mbalimbali vilivyohusianishwa na mahubiri hayo. Vipengele hivyo ni kama vile; uhusiano wa lugha ya mahubiri na wasikilizaji, uhusiano wa mahubiri na mada, kichwa, mifano, ukristo, wakati, na kadhalika. Utafiti huu umefanywa ndani ya wilaya ya Mbeya mjini na kuhusisha waumini wa dini ya Kikristo wenye umri na vyeo mbalimbali vya kihuduma yaani wachungaji, wazee wa kanisa n.k. kutoka madhehebu tofautitofauti walihojiwa. Utafiti huu umetumia Nadharia ya Umanilizi pamoja na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji/Msikilizaji. Nadharia ya Umanilizi ilitumiwa kubaini uvunjifu wa kanuni ya uhusiano na madhara yake katika mahubiri. Wakati, Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji/Msikilizaji ilitumiwa kubaini mitazamo ya watafitiwa/wasikilizaji wa mahubiri juu ya uhusiano wa mahubiri na vipengele mbalimbali vilivyohusishwa nayo. Mwisho, tasinifu hii imethibitisha kuwa mahubiri ya dini yaliyotafitiwa yana uzingativu wa kanuni ya uhusiano kwa kiasi kikubwa na pia yana uvunjifu wa kanuni hiyo kwa kiasi kidogo. Uzingativu huo umetokana na lugha ya mahubiri kuwazingatia wasikilizaji, mahubiri kuizingatia jamii husika, mahubiri kuhubiriwa kwa mitindo ya ufafanuzi wa mada, nukuu ya mada, usimulizi wa mada n.k. Aidha, uvunjifu wa kanuni ya uhusiano pia umejitokeza katika mahubiri hayo na kusababisha madhara mbalimbali, kama vile: maana ya mahubiri kuwa tata kutokana na dhahania mbalimbali juu ya maana ya mahubiri hayo, hivyo mahubiri kuwa na uziada dufu wa maana; maana za mahubiri kupungua au kuongezeka kutokana na kuibuka kwa dhahania mbalimbali juu ya maana za mahubiri; kwa mfano, uvunjifu wa uhusiano wa mahubiri na mada ya mahubiri kulingana na muktadha wa dini kumeibua maana mbadala za mahubiri kutoka kwa wachungaji waliotafitiwa.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.M8524)
Keywords
Swahili literature, Preaching
Citation
Mwalwisi, A.B. (2017) Uzingativu wa kanuni ya uhusiano katika mahubiri ya dini ya kikristo. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.