Asili, maana na uhifadhi wa majina yavijiji: mifano kutoka mkoa wa Kusini Unguja

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza majina ya vijui vinavyopatikana katika Mkoa wa Kusini Unguja. Utafiti ulilenga kueleza asili ya majina ya vim', kufafanua maana ya majina hayo na mwisho kubainisha namna asili na maana majina ya vim' husika inavyohifadhiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia Jumuishi ya Giles (1979). Nadharia hii inafafanua kwamba utambulisho wa mtu au jamii ni mchakato unaoendelea ambao kimsingi unahusisha vibainishi vingi. Vibainishi vya msingi kwa mujibu wa nadharia hii vinaweza kuwa utamaduni, mila na desturi, imani, na kadhalika. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano na hojaji. Ufafanuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maana.Matokeo ya utafiti huu yanabainisha kuwapo kwa sababu mbalimbali zilizotumiwa katika utoaji wa majina ya vijiji katika Mkoa wa Kusini Unguja. Sababu zilizodhihirika ni matukio yaliyotokea katika jamii, sura na tabia ya nchi, tabia za watu, wanyama na miti. Vilevile, utafiti huu umebaini kuwa taarifa kuhusu asili na maana ya majina ya vijui katika Mkoa wa Kusini Unguja zinahifadhiwa kichwani na kwa njia ya maandishi. Kutokana na data za utafiti huu inapendekezwa kwamba tafiti nyingine zifanyike katika uwanja huu wa isimujamii, hususani kipengele cha majina ya mahali. Hii ni kwa sababu bado kuna vipengele vingi katika majina ya mahali ambavyo havijatafitiwa. Vipengele hivyo ni majina ya vitongoji na majengo yanayopatikana katika visiwa vya Zanzibar.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, ( THS EAF PL8704.Z9H344)
Keywords
Swahili language, Unguja, Names, Geographical, Tanzania
Citation
Haji, Zaituni Abdulla (2019) Asili, maana na uhifadhi wa majina yavijiji: mifano kutoka mkoa wa Kusini Unguja .Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.